–Tukizungumzia kuku ni ufugaji wenye faida sana kama ukizingatia utaratibu wa ufugaji, na magonjwa ni moja ya changamoto kubwa katika ufugaji.
Leo tuangalie ugonjwa wa haharisha damu kwa kuku (coccidiosis).
==>Coccidiosis usababishwa na protozoa walio katika kabila la aimeria.sababu kubwa ya ugonjwa huu ni uchafu katika maji na chakula.
Ugonjwa huu ushambulia sehemu za utumbo
Dalili za ugonjwa
-kinyesi cha ugoro au damu kama ugonjwa umekaa sana
-kushusha mabawa kama amevaa koti
-kukosa hamu ya kula
-kupungua uzito
-kupunguza utagaji wa mayai
Kuzuia:
-hakikisha maji safi na vyombo vya chakula na maji viwe safi wakati wote
-epuka unyevu kwenye maranda
-usiruhusu wageni kuingia kwenye banda kiholela
-mlangoni pajengwe sehemu ya kuoshea viatu(foot bath) ili kuua vimelea
-hakikisha usafi wa banda
Matibabu:
Dalili zikionekana mapema matibabu yaanze haraka kwa kutumia dawa za kuchanganya kwenye maji kama:-
-anticox
-amprolium20%
-vitacox
-dawa za salfa