Pakua app yako ya Ufugaji HAPA ili uweze kufuatilia elimu hii kiganjani mwako
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa. Ugonjwa huu wa kuhara damu huonekana katika sura mbili.
(1) Caecal coccidiosis Sura hii ya ugonjwa hushika vifalanga na huathiri kwa kiasi kikubwa sekamu (caecum).
Dalili zake
_Vifaranga huonekana wamezubaa, kushusha mabawa
_Kinyesi kuonesha damu
_Vifo vingi hutokea
_Vifaranga kushindwa kula na kunywa.
_Damu huonekana kwa wingi katika kinyesi kabla ya kifo.
Katika sura hii Kifaranga chenye koksidiosisi sio lazima kionesha dalili zote au kinyesi cha damu. Unaweza kuona vifaranga wako wamezubaa, huku wameshusha mabawa vifo vingi kila asubuhi. Basi tambua vifaranga wako wamekumbwa na ugonjwa huu. Usipo kuwa makini unaweza kujiuliza ni ugonjwa gani? Kwa kuwa umezoea mpaka uione damu kwenye kinyesi ndio ujue kuwa ni coccidiosis.
(2) Intestinal coccidiosis Sura hii ya ugonjwa huonekana kwa kuku wakubwa.
Dalili zake
_Kuku kupunguza ulaji wa chakula
_Kuku kupungua uzito
_ Kuku kuangusha mabawa
_Kuku kuharisha kijivu na damu, ugoro na mala nyingi kinyesi huwa kimechanganyikana na damu damu
_ Kuku kukonda
_Utagaji wa mayai kupungua sana.
UKIUPASUA MZOGA
- Utumbo kuonekana na damu
- Utumbo butu kuwa na damu damu
- Utumbo butu kuvimba
- Utumbo sehemu za ndani kuonekana kama vile umesagika,cloaca ya kuku hubadilika rangi na kuwa na vidotidot kama vya damu [hemorrhage]
KUZUIA UGONJWA HUU
_ Epeka hali ya unyevu unyevu katika banda la kuku
_Ni muhimu kizingatia hali ya usafi kwenye banda la kuku ikiwa ni pamoja na usafi wa vyombo vya chakula na maji.
MATIBABU YA UGONJWA WA COCCIDIOSIS
_Ebs3
_Anticox
_Vitacox
_Amprolium
_Dawa za sulfa
Tunawatakia ufugaji mwema
Imeandaliwa na Lukas Michael (lukasmichael811@gmail.com) na Kuhaririwa na Mhariri mkuu wa Tovuti hii