Mafunzo ya ng’ombe kuwa maksai na matunzo yake

Utangulizi

Kitaalamu, tekinolojia ya zana za kilimo imegawanyika katika sehemu kuu tatu. Tekinolojia ya kwanza ni ya kutumia nguvu za mwanadamu kama jembe la mkono. Tekinolojia ya kati ni ya kutumia nguvu za wanyama kama maksai na punda. Tekinolojia ya tatu ni ya matumizi ya mitambo kama trekta na umeme.

Katika Tanzania, tekinolojia mbili za mwanzo ndizo zinazotumiwa zaidi na wakulima. Tekinolojia ya juu haitumiwi zaidi na wakulima kutokana na uwezo mdogo kiuchumi na kitaalamu.

Matumizi ya wanyama kazi ni tekinolojia ambayo husaidia katika kuongeza uzalishaji na kumrahisishia kazi mkulima. Baadhi ya wanyamakazi wanaotumika zaidi duniani ni ng’ombe, punda, farasi ngamia nyati na tembo.

Hapa Tanzania, wakulima wengi wametambua umuhimu wa inatumizi ya wanyama kazi hasa ng’ombe na punda na wamekuwa wakitumia wanyama hao kwa miaka mingi. Kati ya wanyama hawa wawili, ng’ombe wa maksai hutumika zaidi. Mikoa ambayo ni maarufu katika matumizi ya maksai ni Dodoma, Singida, Tabora, Rukwa, Shinyanga, Mwanza, Mbeya, Mara na Iringa. Katika miaka ya karibuni, karibu Mikoa yote ya Tanzania imeanza kutumia tekinolojia hii katika shughuli mbali mbali.

Pamoja na uzoefu huo ufundishaji na utunzaji wa maksai bado ni dunijambo ambalo linasababisha upungufu katika utumiaji wa huduma hii.

Kijitabu hiki kimelenga katika kumsaidia mkulima kuelewa zaidi tekinolojia ya kati ya zana za kilimo.

Kuchagua Ng’ombe wa kuwa Maksai

Ng’ombe anayefaa kuwa maksai lazima awe na sifa zifuatazo:-

– Awe na umri kati ya miaka miwili hadi mitatu. Iwapo ng’ombe ni chotara, umri wake uwe kati ya mwaka mmoja na nusu hadi miwili.

– Awe na afya nzuri

– Awe na miguu iliyonyooka mbele na nyuma (asiwe na matege), kwato imara, kifua kipana, mgongo ulionyooka, pembe fiipi, shingo fupi na nene.

– Awe na nundu ya wastani.

– Awe mchangamfu

– Awe ng’ombe wa kienyeji au chotara

– Awe dume aliyehasiwa. Kama ng’ombe hakuhasiwa, ahasiwe mwezi mmoja hadi miwili kabla ya kuanza mafunzo. Kazi ya kuhasi ng’ombe ifanywe na mtaalam wa mifugo.

– Awe mwenye kimo, uzito na umri ambao ni sawa na mwenzake atakaye fundishwa naye.

Kumbuka:

Ng’ombejike ambaye ni tasa anaweza kutumika kama mnyama kazi.

Kuwafundisha Ng’ombe kuwa Maksai

Katika kuwafundisha ng’ombe kuwa maksai, yapo mambo muhimu ya kuzingatia ili kufanikisha kazi ya ufundishaji. Mambo hayo ni; kuwa na mkufunzi, vifaa na mbinu za ufundishaji.

Sifa za Mfundishaji/Mkufunzi

– Aipende na kuilewa kazi yake
– Awe mkakamavu na mwenye nguvu
– Asiwaogope wanyama wake, aonyeshe kuwamudu na kuwadhibiti ipasavyo
– Awe mvumilivu
– Asiwapige wanyama bila sababu
– Awe anatoa amri fupi, sahihi, zinazoeleweka wakati unaostahili na zisibadilishwe.
– Awe anatoa amri kwa sauti inayosikika.

Vifaa

– Nira yenye urefu wa sentimita 150 (futi tano)

– Kamba imara yenye unene wa sentimita moja na nusu mpaka mbili.

– Gogo lenye umbo la Y na uzito usiopungua kilo 10 hadi 20 kutegemea nguvu za ng’ombe.

 

 

– Ng’ombe wawili wenye sifa zilizotajwa awali.

 

 

Mbinu za kuwafundisha Ng’ombe

Hatua zifaatazo zinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuwafundisha ng’ombe.

– Wafundishe ng’ombe kuzoeana kwa kuwafungia pamoja kamba shingoni. Hakikisha kuwa urefu wa kamba kati ya shingo ya ng’ombe mmoja na mwingine ni sentimita 50 mpaka 75. Ng’ombe wapewe majina na wazoeshwe kuitwa kwa majina yao kama vile Masika na Vuli


Ng’ombe waliofungwa kamba ya urafiki

– Ng’ombe wakishazoeana wafangiwe nira shingoni na kuanza kuvuta gogo kwa muda wa siku nne hadi saba na wasibadilishwe katika nafasi zao. Ng’ombe wa kulia abakie kulia na wa kushoto abakie kushoto.

– Gogo la kufundishia huanzia kilo 10 na uzito huongezewa taratibu siku hadi siku mpaka kufikia kilo 70 wakati wa kumaliza zoezi hilo. Umbali kati ya gogo na miguu ya nyuma ya ng’ombe iwe sentimita 60.

– Ng’ombe wafiindishwe kutii amri za kuwaongoza kama vile pinda kulia, pinda kushoto, simama, njoo, nenda mbele na ingia kwenye mtaro. Amri ziwe fupi na zitolewe kwa sauti inayosikika.


Maksai wanaofanya zoezi la kuvuta gogo

– Muda wa kuwafundisha ng’ombe hadi waelewe vizuri ni majuma matatu hadi manne tangu kuanza kufungwa kamba ya shingoni.

Kumbuka:

 

Maksai, wanaofanya kazi wakifungvva pamoja na ng’ombe wanaofundishwa, kazi ya kufundisha inakuwa rahisi na huchukua muda mfupi zaidi. Maksai anayejua kulima, anaweza kufungwa na ng’ombe anayefundishwa iwapo wana sifa zinazolingana.

Leave a Reply