Utitiri na viroboto kwenye banda la mifugo
 1. UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE DISEASE)

 

Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia 90%. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.

 

Kisababishi cha ugonjwa (Etiology)

Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Avian paramyxovirus-1  na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana, kutokuwepo kwa usalama wa viumbe hai (biosecurity) katika shamba lako, uchafu unaoletwa na magari, viatu, vifaa vya kazi, ndege wa porini na watalii

 

Dalili za kideri:

 • Vifo vya ghafla muda mwingine bila hata kuonesha dalili.
 • kuvimba shingo na kichwa
 • Kupooza (paralysis) kwa bawa na miguu
 • Ute hutoka mdomoni na puani
 • Kuku walioathirika hupata kizunguzungu.
 • Kuharisha uharo wa kijani
 • Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka
 • Kuzunguka kama vile ana kifafa
 • Utagaji hushuka na mayai kuwa na umbo lisilokuwa la kawaida (deformed eggs)
 • Zaidi ya 90% ya kuku huweza kufa
 • Kuku hufa kwa kupinda shingo

 

Tiba:

Ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya chanjo tu, lakini unaweza kutumia TRIMAZINE 30% pamoja na Vitamini kwa kuku walioathirika.

 

Kinga:

🔅Ugonjwa huu ukitokea jitahidi kuwatenga kuku wagonjwa na kuku wazima.

🔅Zuia muingiliano wa kutoka banda moja kwenda banda lingine pia weka maji yenye dawa (Farmguard) mlangoni kabla ya kuingia bandani na hakikisha unakanyaga hayo maji yenye dawa.

🔅kideri kinauzuiwa kwa njia  ya chanjo, chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu na mara nne kwa mwaka. (Fuata mtiririko sahihi wa chanjo ya  kideri)

🔅Epuka kuingiza kuku wageni kutoka shamba usilolifahamamu na usilojua kuhusu historia ya chanjo

 

 1. KUHARISHA DAMU (COCCIDIOSIS):

 

Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha protozoa cha jamii ya Eimeria (Eimeria tenela, Eimeria maxima, na Eimeria acervulina).

Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira machafu, kama vinyesi, vyakula vilivyooza na umaji maji au unyevu wa maranda.(moist environments).

 

Dalili zake:

 • Kinyesi cha kuku huchanganyika na damu au rangi ya kahawia
 • Wakati mwingine kuku hunya damu.
 • Kuku hudhoofika sana.
 • Kuku huteremsha mabawa yake.
 • Hatimaye vifo hutokea.

 

Tiba;

Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za

(i) Kundi la suphur

Mfano: Sulphonamides (Esb3), sulfaquinoxaline kwa siku 3-4

(ii) Amprolium au Anticox, Agracox.

 

Kinga:

🔅 Zingatia usafi mara kwa mara, Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu, ni vizuri kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu wakati wote.

🔅Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa walio wazima.

🔅Tumia dawa ya kinga ili kuepusha uwezekano wa kuku kuambukizwa ugonjwa huu

Dawa inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat).

🔅Tenga kuku wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.

 

 1. HOMA YA MATUMBO (FOWL TYPHOID):

 

Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa jamii ya Salmonella kwa njia ya uchafu wa vyombo, maji na chakula. Kutupa mizoga ovyo.

Kimelea hicho cha bacteria kisababishi  huitwa Salmonella gallinarum.

🪐Ugonjwa huu huathiri Kuku wanaokuwa au kuku wakubwa wanaotaga na majogoo.

 

Dalili zake:

 • Uharo rangi ya njano na hubakia kwenye manyoya sehemu ya haja
 • Vifo hufikia kiasi cha 50%
 • Rangi ya minofu hugeuka kuwa ya njano
 • Viungo vya ndani kama maini, figo, bandama huvimba
 • Maini hung’aa kwenye mwanga mkali.

 

Tiba

Tumia dawa za antibiotiki kama vile TRIMAZINE 30% au furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.

 

Kinga

🔅Chanja kuku wako mara kwa mara.

🔅 Fanya usafi wa banda na vyombo vya kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.

 

 1. GUMBORO (INFECTIOUS BURSAL DISEASE):

 

Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho birnavirus. Huu ugonjwa huathiri kuku wa umri chini ya wiki 6. Japo hata wenye wiki 15 inaweza kuwatokea.

Huambukizwa kwa njia ya chakula kichafu na maji.

Vifo vinafika hadi 30%.

 

Dalili zake:

 • Kuku kudonoa sehemu ya haja na kubimba cloaca
 • Uharo mweupe kama chokaa ambao hubakia kwenye manyoya ya nyuma
 • Kiwango kikubwa cha vifo
 • Vifaranga huvaa koti (mabawa hushuka)

 

Tiba

Tenga kuku wagonjwa.

Hamna tiba zaidi ya chanjo, lakini unaweza kutumia antibiotic kama OTC kupunguza makali ya ugonjwa

 

Kinga:

🔅 Usafi wa vyombo na maji safi

🔅lishe bora kwa kuku

🔅 chanja vifaranga wakiwa na umri wa wiki 2 na wiki ya 4 kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)

 

 1. NDUI (FOWL POX)

 

Ugonjwa wa ndui ya kuku mara nyingi huwashambulia kuku wadogo na wakubwa. Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho Avipoxvirus kinakuwa kimebebwa na mbu kutoka kwa kuku mgonjwa na kuambukizwa kwa kuku mzima.

 

Jinsi unavyoambukizwa:

🪐 Ugonjwa huu huambukizwa kwa kupitia kwenye vijeraha vya kuku, macho na pua.

🪐Mbu na wadudu wengine waumao huweza kuambukiza anapomuuma kuku mgonjwa na halafu akamuuma kuku asiye na ugonjwa.

 

Dalili zake:

 • Kupoteza hamu ya kula.
 • Kupoteza uzito.
 • Kutokea kwa vipele sehemu mbalimbali zisizo na manyoya mfano upanga wa kuku, sehemu za macho na miguuni.
 • Baada ya siku kati ya 7 hadi 14 vipele hupasuka na kuacha vidonda.
 • Vifo huweza kutokea kwa kuku wenye umri mdogo.
 • Kutoa kamasi kwenye pua.
 • Mara nyingi vipele husababisha kuziba macho.

 

Tiba

Ugonjwa huu hauna tiba,kwani huambukizwa na virusi. Lakini inashauriwa kuwaosha kwa kitamba na pamba safi  vidonda hivo kwa maji ya vuguvugu uchanganye na chumvi kidogo au muoshee na Iodine tincture  akauke kisha mpe  kuku dawa ya Antibiotic ili kuzuia kutibu magonjwa nyemelezi yanayoweza kuwashambulia kuku kupitia kwenye vidonda. Mfano OTC 50%.

 

Kinga:

🔅Ndui ya kuku huzuiwa kwa chanjo ya ndui kwa njia ya sindano (siku ya 35).

🔅 Vifaranga wapatiwe chanjo wakiwa na umri wa siku moja

🔅Tenga kuku wagonjwa na wazima.

🔅Fukia madimbwi karibu na nyumba ili kuepusha mazalia ya mbu.

 

Muhimu: Ili kupunguza kasi endapo ugonjwa huu umewapata kuku,sugua majeraha au vipele kwa pamba iliyochovywa kwenye dawa ya madini joto (Iodine) na baadaye paka mafuta mazito (Petroleum jelly)au samli.Hii sio kutibu ugonjwa bali unawasaidia kuku kulainisha ngozi na macho yapate kuona chakula na maji.

 

MATATIZO YATOKANAYO NA LISHE DUNI KWA KUKU (Nutritional and Metabolic Disorders):

 

✍️ Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho vinavyokosekana mwilini

Kwa mfano:

1️⃣Kupinda miguu (rickets): husababishwa na upungufu wa Vitamin D, madini ya calcium na fosforasi.

2️⃣ Vidonda vyenye damu husababishwa na vitamin K

3️⃣  Kichaa cha kuku na kusinyaa kwa misuli: husababishwa na upungufu wa Vitamin E

4️⃣Magamba ya Mayai (egg shell): kuwa laini ama umbo kuwa bovu husababishwa na upungufu wa madini ya calcium na fosforasi.

5️⃣  Kudonoana: kusababishwa kwa njia moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya chuma, fosforasi na calcium

6️⃣ Kuvimba macho, upungufu wa damu:  huletwa na upungufu wa vitamin A.

 

Kinga:

🔅 Kuwapa kuku mlo kamili

🔅Kuelewa kwa kina aina za chakula kwa kila rika na aina ya kuku; vifaranga, kuku wa mayai na wa nyama. (Poultry age and classes i.e chicks, layers and broilers)

🔅Kufanya uchunguzi wa virutubisho vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.

 

 1. MINYOO (HELMINTHIASIS):

 

Minyoo iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba, minyoo bapa na minyoo ya mviringo

 

Dalili zake:

 • Kudumaa
 • Kuwa manyoya hafifu
 • Kupungua uzito
 • Kukonda, Manyoya kuwa rafu
 • Manyoya hunyoyoka
 • Minyoo huonekana kwenye kinyesi cha kuku pia

 

Kinga na kuzuia minyoo:

✍️ USAFI:

🔅Fanya usafi wa vyombo, banda na mazingira.

🔅Tenga vifaranga kutoka kwa wale wakubwa.

🔅Badilisha matandazo kuondoa mazalia ya minyoo.

 

Tiba

 • Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile zinazoua minyoo ya aina zote (mfano: piperazine citrate, Levamisole
 • Hakikisha kila baada ya miezi 2 au 3 unawapa kuku wako dawa za minyoo.

 

 1. KUPE, UTITIRI, CHAWA NA VIROBOTO

 

Kupe laini waitwao Argus persicus, chawa na viroboto wanaong’ata mara nyingi wanakuwepo kwa kuku

 

Dalili zake:

 • Kujikung’uta na kujing’ata muda wote hatulii
 • Utagaji hukupua kwa kuku wa mayai
 • Kupiga kelele.
 • Kiasi cha damu hupungua mwilini.
 • Utando wa ngozi ndani ya kope za macho hupauka.
 • Utando wa ngozi ya juu mwilini huwa mnene.

 

 • Magamba ya unga-unga hudondoka.

 

Kinga

🔅 Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.

🔅Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa; kuna dawa zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyizia kwenye banda la kuku. Mfano wa hizo dawa ni SEVIN, ANKHERI POWDER n.k (Dawa hizi ni za unga).

 

Mfugaji ukihitaji kitabu pdf kilichoelezea vizuri na picha zake halisi za magonjwa nitafute kisha utalipia 5000 alafu nakutumia kwa whatsap au Email.

 

@ben kukufarm

0625728535

 

🙏🙏🙏🙏🙏

Leave a Reply