Wajue kuku aina ya kuroiler na sifa unazotakiwa kuzifahamu

Kuroiler ni mchanganyiko wa kuku wa aina mbili. Ni mchanganyiko wa Jogoo wa broiler (Kutoka Sasso). Hawa Sasso wanakuwa na umbo kubwa na kuongeza uzito (nyama).
Akapandishwa Jike wa Rhodes Island Red huyu anasifa kubwa kwenye utagaji wa Mayai.
Kwahiyo Kuroiler ni kuku mwenye sifa za kuwa na uzito mkubwa (kutoka kwa baba) na Mayai mengi (kutoka kwa mama).

Hivyo basi kama wewe ni Mfugaji na unataka kupata kipato kupitia kuku

 

Kwanini ufuge Kuroiler

Kuroiler ndio kuku mwenye faida kuliko kuku mwingine yoyote
fuga

Sababu za kwanini ufuge Kuroiler ni pamoja na:
1. Anakua kwa haraka Zaidi (Karithi kwa Jogoo)
2. Anataga Mayai mengi zaidi (karithi kwa mama)
3. Ana kuwa na uzito mkubwa zaidi ya kuku mwingine. Jogoo anaweza kufikisha kilo 5 katika miezi mitano wakati kuku wengine wa kienyeji wanafika kilo 3 Baada ya Mwaka mmoja.
4. Mayai ya Kuroiler na nyama yake ni Bora zaidi. Mayai yana kiini cha njano na radha nzuri sana.
5. Gharama za kuwatunza ni za kawaida kabisa: unaweza ukamuachia akajitafutia chakula mwenyewe.

 

VIDEO YA KUROILER

 

Sifa 7 kubwa za Kuroiler ambazo watu wengi hawazijui.

  1. Unaweza kuwafuga katika mazingira ya kawaida

Unaweza kuwafuga kama kuku wa kienyeji au ukawafuga kisasa kwa kuwaweka ndani ya banda ila wawe huru.

Inamaana hata gharama za kuwa hudumia ziko chini sana ukilinganisha na kuku wengine.

 

  1. Kuku hawa ni wastahimilivu wa magonjwa

Hivyo uwezekano wa kupata hasara kupitia magonjwa ni mdogo

(kama utawapatia chanjo kwa wakati na chakula kizuri na kufuata kanuni bora za ufugaji kuku)

 

  1. Kuroiler huanza kutaga wakiwa na Miezi 5 tu!

(Tofauti na kuku wa kienyeji wa hapa nchini ambao huanza kutaga wakiwa na miezi 6)

 

  1. Kuroiler hutaga mfululizo kwa muda wa miaka miwili.

(Yani utauza mayai mpaka uchoke wewe)

 

  1. Kuroiler ni wazuri kwa nyama pia kwa maana majogoo hufikisha uzito wa hadi Kilo 5 na Mitetea hufikisha kilo 3.5 hadi 4.

 

  1. Mayai yao yana yana mbegu na yanaweza kutotoleshwa

Ila hawalalii, inamaana ukitaka kutotolesha inabidi uatamize kwa kuku wengine wa kienyeji.

Au utumie mashine (Incubators) amabazo tunazo pia na unaweza kuzipata kwa gharama nafuu.

 

  1. Soko la kuku hawa ni kubwa mno kwa maana ni wazuri kwa mayai na nyama

 

Leave a Reply