Hili ni banda la nguruwe ambalo limegawashwa katika maeneo makuu mawili; Eneo la mwanzo ni la nguruwe wakubwa kuanzia wale walioacha kunyonya na eneo la pili ambalo lonaunganisha sehemu iliyoezekwa ni kwa ajili ya kuzalia na kulea watoto wakiwa wadogo. Na ndani ya sehemu ya kuzalia kuna vyumba vidogo ambavyo watoto hufungiwa huko wakati fulani kuepusha mama asiwalalie.
Nguruwe ananyonyesha mtoto na wengine wakiwa wamelala kwa pamoja pembeni ya mama yao. Tazama wana mchanganyiko wa rangi, nyeupe, nyeusi na kahawia rangi ambayo ni adimu kuikuta hasa hapa kwetu. Chini zimetandazwa nyasi raini ambayo yanasaidia kuwapa joto na wasiumie kwenye sakafu. Nyasi hubadilishwa kila zinapokuwa zimeharibika au kuwa na unyevunyevu.
Huyu ni nguruwe dume akiwa na nguruwe wengine wa umri wa kati. Hapa wapo kwenye eneo lililojengewa uzio kuwapa uhuru wa kutembea kwa kiasi fulani huku wakikitafutia chakula chao kama ufugaji huria. Uzio huu umeunganishwa na banda ambapo wanakuwa huru kuingia na kutoka ndani ya banda lakini si nje ya uzio. Ni ufugaji mzuri kwani unawasaidia nguruwe wafanye mazoezi ya kutembea na kukimbiakimbia kwa uhuru mkubwa. Pia ufugaji huu unasaidia nguruwe kupata madini ya chuma kutoka kwenye udongo.

 

TAZAMA VIDEO ZA UFUGAJI WA NGURUWE

  1. BANDA LA KUFUGIA NGURUWE
  2. NGURUWE WAKILA NDANI YA UZIO

 

Leave a Reply