Ufugaji wa nguruwe: mambo muhimu ya kuzingatia kwa nguruwe wachanga

Nguruwe moja jike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:

 Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini (Iodine) 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.

 Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie balbu za joto.

 Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatu baada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu. Hii ni muhimu kwa Nguruwe wanaofugiwa kwenye sakafu iliyowekwa simenti au kujengwa kwa changarawe. Nguruwe wanaofugwa kwenye banda la udongo sakafuni madini haya ya chuma huyapata kwa kula udongo.

 Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.

 Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.

 Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao

 Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.

 Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo

 Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.

 

KUWAACHISHA WATOTO KUNYONYA

Hili ni zoezi la kuwatenganisha watoto na mama yao halitakiwi kufanywa kwa ghafla. Fanya taratibu na kwa makini ili kutowapa watoto mshituko. Wanatakiwa wazoeshwe kula vyakula vigumu taratibu kabla ya kuachishwa kama ilivyoelekezwa hapo juu. Watoto wanatakiwa waachishwe kunyonya kwa kuzingatia uzito wao na sio umri wao.

Ni vyema kuwaachisha watoto kunyonya wakiwa na uzito wa kilo 9 – 11. Kama watoto wamelelewa vizuri watafikia uzito huo wakiwa na umri wa siku 58 (Takriban miezi miwili). Kama watoto watakuwa na uzito chini ya kilo 9 kwenye umri wa miezi miwili inaashiria kuwa walipatiwa matunzo duni.

Baada ya kuwaachisha watoto kunyonya wanatakiwa kupatiwa mahali pazuri pa kukaa, penye nafasi ya kutosha, na kuwe na vyombo vya chakula na maji. Usiweke kundi kubwa la watoto (mfano zaidi ya watoto watatu) uliowaachisha kunyonya kwenye banda moja. Ni vyema watengwe kati ya majike na vidume

Watoto uliowaachisha wanatakiwa kulishwa chakula kidogo kidogo lakini kwa mara nyingi

 

UFUGAJI BORA WA NGURUWE WASILIANA NASI 0719549848, 0762357135

Leave a Reply