Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Na Patrick Tungu 

Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula yaani mbonga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.

Nguruwe hutegemea sana mambo yafuatayo;
1. Bada imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika bada la Nguruwe

3. Mchaganyo bora wa chakula

4. Tiba bora na kinga

5.  Maji na Lishe (upatikanaji wa vyakula muhimu kwake)

Faida ya ufugaji wa nguruwe

Faida kuu ni zao la chakula lakini pia ni zao lenye kukuongezea kipato

Lengo langu nikueleza namna tunavyoweza kufuga na kupata faida
Hatua zifuatazo ni muhimu kuzigatia

JIPE MTAJI WA MILLION 3

Uandaaji wa bada (weka makadilio ya laki tano)

Mfano.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya sh.5,000/= mfano mabati 20 ya futi 10 /10 utapata kwa 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa sh. 2,000/= kila moja utapata mabazi 50 kwa sh. 100, 000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya sh. 1, 000/= na 2,000/= miti ya 50,000/= inatosha sana
4. Tafuta chagalawe trip kazaa na cement mifuko 3 na misumari ambavyo vitagharimu sh. 100,000/= kwa vyote.
5. Malipo ya fundi 50,000/= fundi uashi na 50,000/= fundi seremala

50,000/= inayobaki ni kwa ajiri ziada kwa matumizi mbalimbali

Jumla hapo utatumia laki tano sh. 500,000/=

Ununuzi wa nguruwe wa kuanzia
Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu.

Chukua mfano MILLION 2.

Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano.

Milioni 2 inakupa vitoto 40 au 45.
Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 40 baadaye ukaleta madume matano na au ukawa na vitoto jike 40 na vidume 5 baada ya muda fulani vikikuwa unaongeza Madame matano makubwa.  Either ya kuazima au kukodi.

Maandalizi ya chakula

Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwenye laki tano iliyobaki, tiba / kinga,  lishe na excess zinazoweza jitokeza

Kipato au faida ya ufugaji nguruwe

Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa.
Katiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 40 utatupa faida kama ifatavyo

Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka name huzaa watoto zaidi ya watano.

Basi chukua nguruwe 40 *5 = 200 ukijumlisha na wake 40 wa mtaji umakuwa nao 240.
Chukua zao la nguruwe la 200 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 40.

Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 40 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 40 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili.

Je ukikipa mwaka na miezi 6 kwa mtaji wako wa million 3 utakosa million 80?
Lazima upate million 80.

NB. Jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia lengo.
CHUKUA KALAMU NA KARATASI FANYA HESABU MWENYEWE KWA MTAJI WAKO NA NAMNA UNAVYOWEZA USIPOPATA FAIDA NIPIGIE SIMU PIA UKIPATA FAIDA NIPIGIE SIMU KWA MAELEZO ZAIDI NA MSAADA ZAIDI.

Pia kwa wale wanaohitaji kufanya hii project hawana eneo wala uhakika wa chakula na lishe tuwasiliane kwa msaada zaidi.
KARIBUNI

Patrick Tungu sociologist
Patricktungu12@gmail.com

  1. / 0716063424

Leave a Reply