Jinsi ya kutengeneza funza kwa chakula cha kuku

Na Dua Ramadhan

Moja ya virutubisho muhimu vya kuku ni protini ambayo unaweza kuwapa kupitia vyakula mbalimbali.  Funza ni wadudu walio na protini nyingi ambayo inahitajika sana kwa ajili ya ukuaji wa kuku.

Zipo njia mbalimbali ambazo zinatumika kutengeneza funza na hivyo kupunguza gharama za vyakula vya kuku.

HATUA ZA KUTENGENEZA FUNZA

  1. Tafuta kinyesi cha kuku au mavi ya ng’ombe ambayo unaweza kuyapata machinjioni au toka kwa kuku wako mwenyewe.
  2. Chukua kinyesi weka kwenye kidumu kilichokatwa kisha weka pumba za mahindi kwa juu.
  3. Kisha weka maji kidogo ili kuvutia nzi waweze kutaga mayai. Utaendelea kuweka maji hapo kwa siku 2 na kisha uache siku ya tatu, siku ya nne au tano funza wataanza kutokea.
  4. Wakusanye funza waliozalishwa kwenye kidumu chako
  5. Waoshe na kisha wape kuku wako wale.

Wajua kuwa funza waliokaushwa wanauzwa kuazia kilo 1 kwa sh 35, 000/= kwa ajili ya kuku, bata, na samaki? Kwa Kenya kuna kampuni inazalisha tani laki 4 za funza kwa mwaka. Hii ni fursa nzuri kwa mufugaji kuzalisha mwenyewe kuepuka kuingia gharama zisizo za lazima.

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!