Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi. Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-

  • Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
  • Kujenga banda au zizi bora.
  • Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
  • Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
  • Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
  • Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo
  • Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
  • Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
  • Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.

 

Chanzo: TAVETA

Leave a Reply