UPUNGUZAJI WA MIDOMO YA KUKU
- Maana.
Ni uondoaji/ukataji wa sehemu ya ncha ya mbele kwenye upande wa juu na wa chini wa mdomo wa kuku.
- Kwa nini kuku hupunguzwa mdomo?
* Kuzuia kuku kudonoana manyoya na ngozi, inayoweza pelekea vifo vya kuku kwa 25% – 30% kwenye kundi la kuku.
* Kuzuia ulaji/uvunjaji wa mayai.
* Kuzuia majogoo kuumizana wakati wa kupigana.
- Njia za upunguzaji midomo ya kuku.
* Kwa kutumia mikasi maalumu ya kukatia midomo.
* Kwa kutumia mashine ya umeme yenye wembe wa joto.
* Kwa kutumia kisu cha moto.
* Kwa kutumia mashine yenye mionzi.
- Midomo ya kuku ipunguzwe wakiwa na umri gani?
Upunguzaji wa midomo hufanyika wakiwa na umri tofauti tofauti kulingana na matakwa ya mmiliki wa kuku. Inaweza kuwa wakiwa na:
* Siku moja.
* Siku 5 – 10.
* Wiki 4 – 6.
* Wiki 8 – 12.
* Wakubwa (Wanaotaga)
- Faida za kupunguza midomo ya kuku.
* Kupunguza / kuondoa uwezekano wa kuku kudonoana manyoya na ngozi.
* Kupunguza / kuzuia kuku kula mayai.
* Kupunguza / kuzuia majogoo kuumizana wakipigana.
- Madhara ya kupunguza midomo kuku.
* Kuku wanaweza kupata stress/mshituko kutokana na maumivu wakati wa kupunguzwa midomo, hivyo kupelekea kupungua kwenye ukuaji wao au wanaotaga kupunguza kutaga.
* Kushindwa kula chakula na kunywa maji vizuri. Kuku anakula kwa kudonoa chakula, akipunguzwa mdomo vibaya anaweza kushindwa kula na kisha atadhoofika na hata kupelekea kifo.
- Nini kifanyike ili kupunguza uwezekano wa kuhitaji kuwapunguza kuku midomo?
* Kuku waachiwe kwenye eneo la kutosha ili waweze kuparua na kudonoa donoa chini. Hii itawapatia kazi ya kufanya na hivyo kutokudonoana.
* Kuku wapewe chakula bora chenye virutubisho ili kuzuia kudonoana wakitafuta protein.
* Kuku wavalishwe vifaa vinavyozuia kuona mbali, kama miwani ya kuku.
- Sheria ya upunguzaji midomo ya kuku kwenye nchi mbalimbali.
* Australia – Baadhi ya majimbo yanakataza upunguzaji midomo ya kuku, na kwenye majimbo mengine kama Victoria na New South Wales bado kuna mazungumzo kama ikatazwe au la.
* Denmark – Upunguzaji wa midomo ulikuwa unafanyika mpaka mwaka 2014 ilipokatazwa.
* Sweden, Finland na Norway – Hairuhusiwi kukata midomo ya kuku.
* Germany – Waziri wa Kilimo ametangaza kwamba Ujerumani wanaweza kutoa katazo la kupunguza midomo ya kuku mwaka huu 2017 kutokana na masuala ya ustawi wa wanyama.
ZINGATIA: Watu wanaotakiwa kuwapunguza kuku midomo ni wale tu wenye ujuzi huo, na watumie njia sahihi za kuwapunguza midomo, bila kumuathiri kuku mlengwa.
Imeandaliwa na
Aquinus Poultry Farm.
0655347932