Tofauti kati ya ugonjwa wa avian leukosis na mareksiAvian leukosisTofauti kati ya ugonjwa wa avian leukosis na mareksi

Mfanano:

Magonjwa haya yanafanana sana kwa kuwa na viuvimbe vya kansa vyenye muonekano wa rangi ya kijivu kwenye ini, bandama, figo. Mwishoni mwa kukaribia kufa kwa magonjwa yote huonyesha dalili ya kukonda na kuharisha kinyesi cha rangi ya kijani.

 

Utofauti:

Umri: Avian leukosis dalili huanza kuoneka kuku wakiwa na umri wa kuanzia wiki ya 14-16 na kuendelea wakati Mareks dalili huanza kujitokeza kuku wakiwa bado wadogo kuanzia wiki ya 3 lakini mara nyingi kuanzia wiki ya 12 na huwapata hadi kuku wakiwa wiki ya 25 na si Zaidi ya hapo.

Dalili: In la Avian Leukosis huwa limevimba sana kiasi cha hata tumbo la kuku kuonekana limevimba wakati Mareks ini halivimbi sana. Viuvimbe vya kansa kwa Mareks husambaa kwenye viungo vingi Zaidi ikiwemo macho (husababisha upofu), kongosho, mapafu, sehemu ya mbele ya moyo, kwenye ngozi na mfumo wa fahamu. Hii ya mfumo wa fahamu hutofautisha na Avian Leukosis kwa kuku ulemavu wa kushindwa kutembea (huyumbayumba) na kupooza. Kwa Avian Leukosis viuvimbe huenda pia kwenye basa kitu ambacho kwa Mareks hakitokei.

Mareks3 Mareks2 Mareks1

Hawa ni kuku wakionyesha dalili ya Mareks wakiwa wamenyonga shingo zao

Avian Leukosis
Hili ni ini lenye ugonjwa wa Avian Leukosis likiwa limevimba kupita kiasi na viuvimbe vya kansa

Kinga: Magonjwa yote mawili hayana tiba, wakati Avian Leukosis hauna chanjo pia, ugonjwa wa Mareks una chanjo. Kuku wanatakiwa wapewe chanjo ya kwanza wakiwa bado vifaranga na wazalishaji wa vifaranga.

Leave a Reply