Anza kwa Kupakua App ya Ufugaji HAPA

 

Pamoja na kuwapatia huduma bora kuku wako, kuwakinga na wanyama na ndege wanaoweza kuwadhuru iwe ni kitu cha muhimu kwenye vitu unavyopaswa kuvifanya mfugaji.

Mambo ya kufanya ili uwakinge kuku wasidhuriwe.

  1. Jua wanyama na ndege waharibifu waliopo katika eneo lako. Wanaweza kuwa panya, kicheche, fisi, mbweha, nyoka, tai, kunguru, mwewe na kadhalika.
  2. Zungushia waya mgumu kwenye sehemu za wazi za banda. Usiache hata sehemu ndogo wazi.
  3. Hakikisha kuku wameingia bandani kabla ya giza kuingia, na funga mlango kwa kufuli, na hakikisha hakuna uwazi wowote kati ya mlango na banda.
  4. Sakafia banda lako kwa sementi kali ili wanyama wanaofukua chini kama panya wasiweze kufukua na kuingia ndani ya banda.
  5. Kuwe na mtu wa kuwaangalia kuku mchana wanapokua wanazunguka zunguka nje ya banda, ili wanyama au ndege waharibifu wakija waweze kufukuzwa.
  6. Kuwa makini na wanyama wengine unaowafuga kama mbwa na paka, wanaweza kuwadhuru kuku na vifaranga vyako. Kamwe usiwaache peke yao na kuku au vifaranga, mpaka uwe na uhakika kwamba wanaaminika na hawatawadhuru. Pia kuwa makini na mbwa na paka wa majirani, wanaweza kuwadhuru kuku na vifaranga vyako.
  7. Tumia mbwa walinzi wakati unawafungulia kuku nje. Mbwa hawa wanasaidia kuwafukuza wanyama na ndege watakaotaka kuwadhuru kuku.
  8. Tumia teknolojia kulinda kuku wako. Mfano, unaweza kufunga camera na sensor inayoweza kuhisi wanyama wanaotaka kuingia bandani, kisha inapiga kengele au inakujulisha kupitia simu yako.

 

Imeandaliwa na

Aquinus Poultry Farm.

0655347932

Leave a Reply