Njia ya kutengeneza lishe bora ya asili kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa kwa gharama nafuu

ByChengula

Nov 21, 2015 ,
Njia ya kutengeneza lishe bora ya asili kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa kwa gharama nafuuChakulaNjia ya kutengeneza lishe bora ya asili kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa kwa gharama nafuu

Na Mkulima Mbunifu

Lishe bora

Ng’ombe hawezi kulaumiwa kwa kushindwa kufanya urutubishaji. Ukosefu wa lishe sahihi husababisha ng’ombe kuwa dhaifu na pia husababisha kutokea kwa magonjwa ambayo huweza kuathiri mfumo wa uzazi.

 
Mali ghafi zinazotumika kutengeneza chakula cha mifugo nyumbani

Kupungua kwa ulaji wa vyakula vya kutia nguvu huathiri joto na hatimae kupunguza uwezo wa uzalishaji kwa ng’ombe. Hii ina maana, lishe hafifu kwa ng’ombe wa maziwa husababisha ng’ombe kutokupata joto kwa wakati uliotarajiwa kwa sababu miili yao haipo katika hali nzuri ya kubeba mimba. Ng’ombe lazima alishwe mlo kamili unaojumuisha wanga, protini, madini na vitamini.

Utafiti unaonesha kwamba ng’ombe aliyeathirika kutokana na utapiamlo, baada ya mwili wake kujijenga kwa upya na kuwa katika hali ya kawaida, huweza kujirudia katika hali ya uzalishaji na akashika mimba kwa haraka sana hata kuliko ng’ombe aliyekuwa akipata mlo kamili kwa wakati wote.

Uzalishaji wa lishe
Ng’ombe anayelishwa nyasi tu hawezi kufikia kiwango kizuri cha uzalishaji maziwa hivyo anahitaji kupatiwa lishe ya ziada. Virutubisho vya ziada kama vile dairy meal inakadiriwa kugharimu asilimia20% zaidi ya gharama ya jumla ya uzalishajiwa maziwa, hivyo kupunguzafaida kwa mfugaji.

Kuongeza virutubisho vinavyochochea uzalishaji wa maziwa kwa kutumia lishe ya asili inayopatikana kwenye mazingira ya mfugaji na yenye gharama nafuu husaidia wafugaji kupata maziwa mengi kwa gharama ya chini. Ili virutubisho vya ziada kuwa na manufaa kwa ng’ombe ni lazima uwepo uwiano wa upatikanaji wa nishati, protini na madini.

Vyanzo vya wanga: Mahindi, makapi ya ngano, molasesi, pumba ya mahindi, na pumba ya ngano.
Vyanzo vya protini: Nyasi, mbegu za pamba, soya, mbegu za alizeti, majani ya sesbania, majani ya kaliandra, na dagaa.
Vyanzo vya madini: Kalishamu, fosifeti, mawe ya chokaa, pamoja na madini ya premix.

Namna ya kuchanganya virutubisho vya uzalishaji wa maziwa

1. Uzalishaji wa kawaida
Kufanya mchanganyiko wa kilo 100;
• Kilo 75 ya lishe ya wanga
• Kilo 23 ya lishe ya protini
• Kilo 2 za madini
Kwa mfano;
• Kilo 57 za mahindi
• Kilo 18 za makapi ya ngano
• Kilo 17 za lusina
• Kilo 6 za soya
• Kilo 2 za fosifeti

2. Uzalishaji wa maziwa kwa kiwango cha juu

Kufanya mchanganyiko wa Kilo 100;
• Kilo 68 za lishe ya wanga
• Kilo 30 za lishe ya protini
• Kilo 2 za lishe ya madini

Kwa mfano;
• Kilo 50 za mahindi
• Kilo 16 za makapi ya ngano
• Kilo 2 za molasesi
• Kilo 14 za mbegu za pamba
• Kilo 12 za lusina
• Kilo 4 za dagaa

Faida za mchanganyiko unaotengenezwa kiasili

• Una ubora sawa na lishe zinazouzwa.
• Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na lishe ya kununua.
• Hukubalika kwa ng’ombe.
• Ni rahisi kutunza na kutengeneza.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Dkt Emmanuel Mbise kwa simu namba +255 755 807 357.

Leave a Reply