Changamoto ni mtaji katika ufugaji wakoKukuChangamoto ni mtaji katika ufugaji wako

JE, CHANGAMOTO ZINAKUSAIDIA KUKUA KATIKA UFUGAJI WAKO? USIKATE TAMAA

 

Kila jambo katika maisha linachangomoto zake na zinatofautiana. Hivyo hata ufumbuzi wa changamoto hizo unatofautiana sana. Kikubwa usikate tamaa maana ndio mwanzo wa kafanikio katika mradi wako yalipo. “KIKUBWA USIKATE TAMAA”.

Moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwenye mradi ni tabia ya KUACHANA na mradi unapokubwa na CHANGAMOTO. Yaweza kuwa changamoto imesababishwa na uzembe/makosa yako mwenyewe. TAZAMA KILICHOKUANGUWHA na kiondoe kisikuangushe tena siku za mbeleni. Siku zote changamoto iamshe ari ya kufanya vizuri zaidi. Mara nyingi matanikio huja baada ya vikwazo/changamoto. Navyo unavyokabiriana navyo bila kukata tamaa ndo mwanzo wa mafanikio.

Jifunze kuzitatua changamoto bila woga, woga ni adui wa maendeleo. Sisemi utatue changamoto kichwa kichwa. La hasha. Ukipata changamoto waweza kutumia njia zifuatazo kutatua

 

  1. Kuwa mtulivu na kuijua changamoto yako vizuri ikiwa ni pamoja na kutafuta chanzo cha changamoto. Kujua chanzo ni hatua muhimu kutatua tatizo. Mfano kuku wako wameacha/kupunguza kutaga mayai. Fuatilia kwa umakini lini wameanza kupunguza na kama kuna mabadiliko yoyote yametokea kwenye chakula au kuonyesha dalili za magonjwa.

Wengi tunapenda njia za mkato kukimbilia kwenye mitandao kutafuta majibu bila kuchunguza mradi wetu. Yaweza kuwa tu mtunzaji hawapi chakula kwa wakati. Majibu ya hili huwezi kuyapata kwenye mitandao au kwa mtu mwingine.

 

  1. Tumia vyanzo vingine kupata maarifa. Vitabu ni vyanzo vizuri vya kujipatia maarifa. Penda kusoma vitabu vya mradi wako, ukipata changamoto kimbilia huko kwanza. Iwe unafuga kuku, mbuzi, samaki n.k  vitabu kwa ajili ya hiyo mifugo. Usipende tu njia rahisi, jielimishe.

Mitandao pia itumie vema kuchota maarifa kutoka kwa watu wengine wenye uzoefu. Penda kupata majibu kwenye midahalo ya wazi mfano kwenye facebook na maundi ya WhatsApp. Ukipenda Chemba ni rahisi kudanganywa.

Soma Vitabu vya ufugaji HAPA

 

  1. Hakikisha kusudi lako haliyumbishwi. Tangu kuanzisha mradi wako unamalengo na ndoto fulani. Kamwe kusiwe na kitu cha kukuyumbisha kwenye malengo yako. Si changamoto, wala ndoto mpya au watu wengine wakutoe kwenye mstari. Hakikisha ndoto yako inatimia. Sukuma ndoto yako kila siku bila kukata tamaa na uone ikikua. Hapa panahitaji nia ya dhati ya ufuatiliaji na msukumo kutoka ndani.

 

JIFUNZE TOKA KWA WAJASILIAMALI HAWA WA UFUGAJI WA SAMAKI HAPA

 

Leave a Reply