Homa ya nguruwe ni ugonjwa unaoenezwa na kirusi na umekuwa ukijirudia rudia kila mwaka kwa wafugaji wengi nchini mwetu. Hadi sasa ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba, lakini ueneaji wake unaweza kudhibitiwa na wafugaji wakishirikiana na wataalamu wa mifugo na serikali. Na hii itawezekana tu endapo wafugaji watajua namna gani ya kuzuia ueneaji wake.
Fuatitia video hii yenye maelezo ya kina yatakayo kufanya upate uelewa mpana wa ugonjwa wa homa ya nguruwe kutoka kwa mtaalamu wa Chuo cha Sayansi ya Tiba ya Wanyama na Binadamu kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro.
Tazama namna wilaya ya Kalambo iliyokumbwa na ugonjwa huu inavyochukua hatua HAPA
Na kama ulipitwa na maelezo ya kina ya homa ya nguruwe yaliyowekwa humu siku za nyuma pitia na jielimishe HAPA
.