Na Mwandishi wetu Lukas Michael

Karibu tena ndugu mfugaji kwenye tovuti yako uipenday ya UFUGAJI ujifunze ili uongeze mradi wako.
Wafugaji wengi wamejikita katika ufugaji kuku wa kienyeji, kuku wa kienyeji ni kuku wazuri na wenye soko zuri. Pia wanasifika katika kuhimili magonjwa; kuku wakienyeji wakiugua wakipatiwa tiba basi hurudi katika hali yao ya kawaida haraka kuliko kuku wengine. Katika ufugaji kuku kuna mifumo ya ufugaji ya aina tatu:

1. Huria
2. Nusu huria
3. Ndani

Katika kila mfumo hapo kuna faida na hasara zake , kwa mfugaji wa kuku wa kienyeji mifumo mizuri kuitumia ni huria na nusu huria.
Tambua kuwa kuku wa kienyeji ni kuku wenye pilika pilika hivyo ukiwafuga kwa kuwafungia ndani utakuwa kama umewanyima uhuru.
Na uwezekano wa kuku kudonoana, kula mayai huwa ni Mkubwa.
Hapa tutajifunza mfumo wa nusu huria, faida zake na jinsi ya kuuboresha ili kuku wako wawe na maendeleo mazuri.

Katika kuutumia mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda yenye hewa ya kutosha na mabanda hayo huwekewa uzio. Uzio unaweza kujengwa kwa kutumia matofali, wavu, miti hata kwa kutumia nyasi au makuti.
Mfumo huu ni mzuri kwa kuku aina zote (isipo kuwa broiler) ila hapa tunaongelea kwa kuku wa kienyeji.
Kuuboresha mfumo huu ndani ya huo uzio unaweza panda majani ambayo kuku hupenda kula. Katika mfumo wa huria kuku huwa huru zaidi huko nje wanako chunga hukutana na majani ya kila aina .  Hivyo kuku wako unapo wafuga kwa nusu huria hakikisha ndani ya uzio wa banda lako kuna kuwa na bustani ya mboga mboga mchicha nk. Pia unaweza panda miti ambayo ni dawa za asili kwa kuku.
1. Mpapai
2. Mlonge longe
3. Aloe vera
4. Mwarobaini
5. Lusina n.k

Katika mfumo huu ni lazima uwe na sehemu ya kulelea vifaranga kwa kuwa vifaranga vinapototolewa huhitaji joto na uangalizi mzuri basi ni lazima kuwepo na Chumba cha Vifaranga. Kuku wako watakapo angua Vifaranga utavilea katika hiko Chumba kwa muda mpaka utakapo ona kuwa wanaweza kwenda kujichanganya na kuku wakubwa katika hiyo sehemu yenye uzio.

Faida za mfumo huu ni kama ifuatavyo:

_Tabia mbaya ya kuku mfano kudonoana hupungua au kutokuwepo kabisa
_Mfumo huu hutumika kwa kuku wenye umri wowote
_Utunzaji wa kuku ni rahisi kulinganisha na ule wa huria.
_Kuku huwa salama na maadui
_ Mfugaji huwapa kuku chakukula ziada na kupata matokeo mazuri
_Ni rahisi kujua idadi yake na kuwa tenganisha kwa makundi
_Ni rahisi kudhibiti kuku na wadudu vimelea vya magojwa
_Kuku hupata mwanga wa jua wakutosha na wakati jua kali hukaa bandani.
_Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa
_Upotevu wa mayai na kuku hupungua
_Ni rahisi kukusanya mbolea
_ Ni rahisi kutunza kumbukumbu
_Ni njia bora kuliko zote kufugia kuku wa asili
_ Hutumika zaidi maeneo yenye makazi mengi ya watu

Hasara za mfumo huu ni kama ifuatavyo:
_Unahitaji gharama za uzio
_ Mfumo huu sio mzuri kwa kuku wa nyama (broiler)
_Matumizi ya muda mrefu katika eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vyovyote vya ugonjwa.

Utumiaji mzuri wa mfumo huu ni kama ifuatavyo:

1. Fanya usafi eneo husika na banda/jipangie utaratibu wakusafisha eneo lote na banda kwa kutumia dawa za kuuwa wadudu (bacteria)
2. Usiruhusu kila mtu aingie ndani ya uzio wa banda lako ikiwezekana weka utaratibu kabla ya kuingia ndani ya uzio  mlangoni kuwepo na dawa ili wanapoingia waweze kukanyaga na viatu vyao ndipo waingie (Disinfectant)
NAKUTAKIA UFUGAJI MWEMA WENYE MAFANIKIO

 

Leave a Reply