Kipima joto itv: kuibuka kwa uchinjaji holela wa mifugo na kuhatarisha afya za walaji

JE MAMLAKA HUSIKA ZINAWAJIBIKA IPASAVYO KUDHIBITI TATIZO HILO?

Hili ni swali la kipima joto kutoka kituo cha utangazaji cha Televisheni ya ITV kikiongozwa na mtangazaji mahili wa ITV Julieth Robert. Fuatilia video hii ya KIPIMA JOTO ITV  ili upate majibu sahihi ya swali hilo toka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania (Dr. Hezron Nonga) na Daktari Mkuu Mwandamizi wa Mifugo Tanzania (Dr. Severin Assenga) toka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na kutoka kwa Moses Fumbi mfanyabiashara wa nyama. Utapata kujifunza mengi yanayohusiana na uchinjaji wa mifugo nchini na taratibu zote zinazotakiwa kuzifuata pamoja na sheria zake zinaongoza uchinjaji wa mifugo Tanzania. Utajifunza pia kuwa kwa nini taratibu za uchinjaji zinatakiwa kufuatwa na zisipofuatwa nini kitatokea. Kazi hiyo ya kuhakikisha utaratibu unafuatwa ni nani anatakiwa kusimamia kwenye aina zote za machinjio nchini. KARIBU.

 

Leave a Reply