Ufugaji wa mende

Na Dua Ramadhan

Ufugaji wa mende ni ufugaji ambayo unapendwa sana kwani nchini china, Denmark na Australia chakula kikuu cha kuku ni mende. Mende upunguza gharama kubwa ya chakula cha kuku kwa asilimia 90%. Kilo moja ya mende kwa ajili ya matumizi ya mifugo inauzwa elfu 70 wakati kilo moja ya mende kwa ajili ya chakula cha binadamu inauzwa shilingi laki moja.

Matumizi ya mende ni chakula cha mifugo kama kuku, bata, sungura,samaki, lakini pia kwa matumizi ya binadamu.

Chakula cha binadamu soko kubwa ni Wachina wakijua unafuga mende wanakuja kutoa oda yoyote kwani zingine zinasafirishwa kwenda kwao China.

Mende hutumika kutengeneza dawa za urembo, dawa ya vidonda vitokanavyo na moto n.k

Kuna zaidi ya aina 4,000 za mende, kati yao 30 hupatikana kwenye makazi ya watu, huku nne kati yao zinafahamika kama wadudu wasumbufu.

Miongoni mwa aina zinazofahamika sana ni mende wa Amerika, ambaye ana urefu wa milimita 30, mende wa Ujerumani mwenye urefu wa milimita 15, na mende wa Asia anayekaribia urefu wa milimita 25. Mende wa kisasa ni wakubwa kidogo kuliko mende wa kale.

Mende-pori

Mende huishi katika mazingira mbalimbali ya duniani. Mende wasumbufu wanaweza kuishi maeneo mengi zaidi, lakini hupendelea maeneo yenye joto, kwa mfano ndani ya majengo. Mende wengi wa kitropiki hupendelea zaidi joto na kwa hivyo katika kanda nje ya tropiki hushindwa kuishi nje ya majengo. Miiba iliyo miguuni mwa mende ilichukuliwa kuwa inaweza kuhisi lakini tafiti zimeonyesha ni mahususi kwa ajili ya kutembelea kwenye mchanga, nyavu na sehemu ambazo ni shida kutembea. Muundo wake wa miguu umechochea sana miundo kadhaa miguu ya mashine/roboti za binadamu.

Mende huacha kemikali kwenye kinyesi chao, vile vile huacha harufu kwa ajili ya kujamiiana na kusongamana mende wengine watafuata njia / harufu hizi ili kufahamu chanzo cha chakula na maji pia kujua mende wengine wamejificha wapi.

Mende huchangamka zaidi usiku na hukimbia mwanga isipokuwa mende wa huko Asia ambao wao hufuata mwanga.

Mende ambao wamefanyiwa utafiti kwa aijili ya ufugaji wa chakula cha kuku, bata, Samaki na binadamu, dawa ya vidonda vilivoungua na moto na kama matumizi ya urembo wa ngozi kwale walimbwene. Ni mende wa Asia ambao wamechanganywa katika mbegu kuu 3 (yaani Asia, Ujerumani na USA katika maaabara na wameboreshwa ili kupata mende wa kisasa wanaojulikana kwa jina la kitaalam kama diploptera punctuate.

UZAZI WA MENDE

Mende hawa aina ya Diploptera puntuate hujamiiana huku wadudu (mende hao) wengine wakiwa wanatizama pande tofauti, na tendo hili linaweza kuchukua saa kadhaa.

Mende jike huhifadhi mayai yao ndani ya miili yao au bila ya kipeto mpaka pale yatakayo anguliwa.

Tunutu wa mende kwa kawaida ni sawa na mende wakubwa isipokuwa hukosa mbawa na viungo vya uzazi vinakuwa havijakomaa. Ukuaji waweza kuwa taratibu kufikia hata mienzi miwili na nusu kama utawapa chakula na maji kwa wakati sahihi ili kuwafanya kushiba na kukua kwa haraka zaidi. Usipo fanya hivyo kwa wakati wanaweza kufikia mienzi 4. Mende hawa huishi miaka 4 na nusu kunzia pale wanapozaliwa mpaka kuzeeka

MAYAI

Mende hawa wa kisasa ndio hutaga mayai mengi zaidi kuliko mende wote duniani kwani mende mmoja hutaga mayai kuanzia 55 mpaka 70 na pia hutaga mara 3 kwa mwaka kama utazingatia sheria za kuwatunza. Na hukaa miezi miwili na nusu ili wawe wakubwa sana kwa ajili ya chakula.

BANDA LA KUFUGIA MENDE

Mabanda ya kufuga mende yapo ya aina nyingi na ukubwa wake hutofautiana kulingana na wewe unataka kufuga wengi kiasi gani. Mimi leo nafundisha kwa wale wafugaji ambao wanataka kufuga mende kama chakula kikuu na pia wanataka kuuza kwa wengine.

Hatua zifuatazo za kujenga banda

  1. Kuandaa eneo maalumu la ufugaji
  2. Kumtafuta fundi kwa ajili ya ujenzi wa banda
  3. Kama unataka kufuga mende wengi sana kwa kuku wako na kuwauzia watu wengine unaweza ukajenga chumba cha futi 11 kwa 12.
  4. Hakikisha hicho chumba kimezibwa mpaka juu yaani kisiwe na dirisha au sehemu yoyote ile ya kutoa mwanga, ila kiwekee taa ndani itakusaidia wakati wa kuingia ndani pindi ukiwapa chakula na kipindi cha mavuno

5.Ukimaliza ujenzi, tengeneza fremu humo ndani ya banda, fremu kama zile za duka za kuwekea vitu dukani, hizo fremu zizungushe chumba kizima huku ukibakiza njia ya kupita.

  1. Weka maboksi mfano treyi ya mayai katika kila chumba cha fremu.
  2. Tengeneza milango miwili yaani mlango wa nje ambao ni wa mbao na mlango wa ndani ambao utakuwa unazipu. Hakikisha hakuna njia ya kupitishia mende yoyote kutoka nje.

JINSI YA KUWAHUDUMIA MENDE

Kwanza tafuta mbegu za mende za kisasa kwani mbegu hizo zimethibitishwa, usije ukachukua mende wa nyumbani ndo ukawafuga kwani wengi wao wanamangonjwa wanaweza baadae wakaua kuku wako wote. Mende wa kisasa wanapatikana kwa bei ya kuanzia elfu 2000 mpaka elfu 3000 kwa kila mende mmoja na bei hiyo inategemea wakala yupi amekuuzia.

Ukishapata mbegu waweke kwenye banda lako, baada ya hapo hakikisha mende wako muda wote unawapa maji (hakikisha maji hayapungui ndani). Pia hakikisha mende wako unawapa chakula cha kutosha kama vile unga wa ugali wa mahindi, muhogo mbichi na viazi mviringo vibichi (hivi vyote vyaweza vikawa hata vibovu). Hakikisha unatenga chombo maalumu cha maji na chakula na viwekwe mahali mmaalumu.

Hapo utakuwa umefanikiwa kuanza mradi wako wa ufugaji wa mende kwa ajili ya chakula cha mifugo na au kuuza kwa matumizi ya binadamu. Naamini umefaidika sana na elimu hii ya ufugaji wa mende, endelea kufuatilia hapa kwa makala zaidi ya ufugaji wa mifugo mbalimbali.

Mende wana manufaa mengi sana kwa binadamu

https://www.bbc.com/swahili/habari/2015/11/151104_mende_manufaa_faida

Mende huchukiwa sana na watu na huhusishwa na uchafu na maradhi. Lakini wajua kwamba wadudu hawa wana manufaa makubwa sana kwa binadamu?

Mjini Havana, nchini Cuba kuna aina ya mende ambao hufugwa kama wanyama vipenzi na hata visa vyao husimuliwa kwenye hadithi, anasimulia Mary Colwell.

Kwenye kisa kimoja, mende kwa jina Martina huwafanyisha mtihani wanaotaka kumchumbia kwa kuwaudhi kila wanapomtembelea.

“Mwaga kahawa kwenye viatu vyao uone watalichukulia vipi hilo,” anapendekeza nyanyake Martina. “Ni muhimu sana kujua mumeo mtarajiwa hufanya nini anapokasirika – mtihani wa kahawa hufanikiwa.”

Kuna aina 4,500 ya mende, na ni aina nne pekee ambao huwa waharibifu.

Wengi hawaishi karibu na nyumba za watu na hutekeleza jukumu muhimu katika ikolojia kwa kula vitu vilivyokufa na vinavyooza.

Mende BBC1 300x198 - UFUGAJI WA MENDE

Baadhi wana sifa nzuri na huishi pamoja na kusaidiana katika kutafuta chakula na makazi. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee.

Wale wazito zaidi, huwa na uzani wa gramu 35, na urefu wa sentimeta 8 na huishi Australia. Wale wadogo zaidi huishi Ulaya na Amerika Kaskazini na wana urefu wa sentimeta moja pekee.

Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.

Mende huwa thabiti sana, na wakianguka huwa wanainuka upesi na kwa urahisi kwa kutumia mabawa.

Miguu ya mende pia imekuwa ikitumiwa na wavumbuzi wanaotengeneza miguu bandia ya kutumiwa na binadamu.

Kuna pia mende ambao wamekuwa wakiunganishwa na kompyuta ndogo inayowekwa mgongoni na kuongozwa kufika maeneo ambayo mwanadamu hawezi kufika.

Mende BBC2 300x189 - UFUGAJI WA MENDE

“Nilipoona hili mara ya kwanza, nilishangaa sana,” mtafiti mkuu katika mradi huo unaoendeshwa katika Chuo Kikuu cha A&M cha Texas, Hong Liang anasema.

Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu.

Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria zinazohangaisha sana watu kwa mfano E. Coli na MRSA ambazo zimekuwa hazisikii dawa.

Hii si mara ya kwanza mende kutumiwa kwa sababu za kimatibabu. Mwanahabari Lafcadio Hearn karne ya 19 alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokuwa wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kutumia mende.

“Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani sana na tiba hii,” aliandika.

Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.

Mende wanahitajika sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kufungua biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.

Mende BBC3 300x169 - UFUGAJI WA MENDE

 Mende hupikwa na kuliwa nchini Uchina

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!