Ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua: hatua ya sita

Uondoaji wa kuku waliokoma/kupunguza kutaga na kuanza upya ufugaji (Wiki ya 80 na kuendelea)

Kuku wazuri wanaweza kutaga vizuri mfululizo kwa kipindi cha miaka miwili baada ya hapo utagaji wao hushuka. Wakifikisha umri huo wa utagaji ni vyema kuanza kuwaondoa kuku wako maana watakuingizia gharama kubwa ya chakula na matunzo mengine huku wakitaga kidogo.

Mpango wa kuwaondoa na kubadilisha kuku wengine wa mayai unaweza ukaugawa katika njia mbili vile utakavyoona inafaa. Njia ya kwanza unaweza kwa kuanza na kuwaleta vifaranga wa kuku wa mayai ili unapofikia ukomo wa kutaga unakuwa na kuku waliotayari kwa kutaga au wanakaribia kutaga. Hii itakusaida uwe na kuku wanaotaga muda wote wa mzunguko wa ufugaji wa kuku wa mayai. Njia hii ni nzuri hasa kama unafanya biashara ya mkataba ambapo mkataba wako ni kuzalisha mayai na kumpelekea muliyeingia naye mkataba wa kudumu bila kukatisha. Kielelezo hapa chini kinaweza kukusaidia ni wakati gani uanze kufuga vifaranga wa kuku wa mayai kwa ajili ya kubadili waliozeeka. Utagaji wa mayai hupungua kadiri umri unavyoongezeka na hatimaye kupungua kiasi ambacho kuendele nao ni hasara kwa kulisha chakula. Unaweza kuanza kuagiza/kuweka oda ya vifaranga kuku wako wanapofikia umri wa wiki 80 au utakavyoona inafaa kulingana na matokeo ya utagaji wa kuku wako. Hii itasaidia kujipa muda wa kuzalisha vifaranga na kuwafuga wafikie hatua ya kuanza kutaga.

Njia ya pili inajumuisha ubadilishaji na uondoaji wa kuku wote wenye umri wa wiki 20 maana utagaji wao huwa umeshuka kiasi cha kutoleta faida tena. Mpango wa uondoaji wa kuku wazee uandaliwe kwa umakini mkubwa ili kuku wako wasiendelee kukuingizia hasara kubwa kwa walisha chakula kwa utagaji mdogo. Uondoaji wa kuku wazee hufanyika kwa kuwauza kwa wafanya biashara wa jumla au wanunuzi wa reja reja. Endapo utashindwa kupata soko mapema basi ni vyema ukabadili chakula kwa kuwatafutia chakula cha bei nafuu ili ili usiendelee kuingia gharama kubwa.

 

Ndugu mfuatiaji wa Makala hizi za ufugaji wa kuku wa mayai endelea kutembelea Tovuti yetu ya ufugaji kwa hatua ya saba itakayohusu kinga dhidi ya magonjwa ya kuku wa mayai na wadudu waharibifu.

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!