Ufugaji wa kuku kwa njia ya kisasa: utagaji na uatamiaji wa mayai

Na mwandishi wetu Lucas Michael
Ndugu msomaji wa Tovuti yetu uipendayo ya UFUGAJI leo nakuletea Makala inayohusu matunzo kwa kuku anayeatamia mayai. Wafugaji wengi hawajali sana mazingira mayai yalipo ya kuku anayeatamia wakidhani kuku mwenyewe atafanya kila kitu. Makala hii inakupa elimu ya nini cha kufanya kwenye eneo analotagia kuku na wakati wa kuatamia. Futana nami kwenye makala hii fupi.

Kuku wanaotazamiwa kuatamia lazima wachunguzwe kwa makini kwa siku mbili kabla ya kuatamia ili kuhakikisha hawana chawa, utitiri au viroboto. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na wasitulie katika viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa vifaranga wachache au kutoanguliwa kabisa kwa vifarnga na kuishia kupata mayai viza. Ikiwa kuku kwa namna yeyote ile kuku au eneo wanaloatamia lina wadudu hao basi nyunyizia dawa ya kuua wadudu hao. Nenda kwenye maduka ya mifugo ukanunue dawa ya kuua wadudu hao.
Kuku kwa ajili ya kuatamia awe na histori ya tabia ya kuangua vifaranga wengi. Hivyo uwe na tabia ya kuwachunguza kuku wako kujua ni kuku yupi anafaa kwa kuatamia kati ya kuku ulionao.

Kwa baadhi ya wafugaji hutumia mashine za kutotolesha vifaranga au kupeleka mayai kwa wenye mashine hizo ili wakatotoleshe mayai ya kuku wao. Baadhi ya wafugaji walio kijijini hii huwa ni changamoto kwani upatikanaji wa mashine hizo huwa si rahisi. Hivyo wengi hutumia ule mfumo wa kumnyan’ganya kuku vifaranga na kumuekea mayai mengine ili aendelee kuatamia. Mfumo huu ni mzuri ila humdhofisha sana kuku yule ambaye yupo kwa ajili ya kuatamia.

Ni kweli kuwa kuku anaetaga hatakiwi kupewa vyakula vitakavyo mfanya awe na mafuta sana. Kwani kuku anaetaga akiwa na mafuta sana hupunguza kutaga au kuacha kabisa.

Wafugaji wengi, kuku punde aanzapo kuatamia husahau kuwabadilishia mfumo wa chakula na utaratibu wa kuwalisha. Kuku anae atamia hasa yule ambaye akitotoa anawekewa mayai mengine chakula chake kinatakiwa kiwe na virutubisho vyote wanga, madini na protini ili kumfanya awe na nguvu ya kuendelea kuatamia bila kudhoofika . Ni vema kuku wanao tumiwa kuatamia wawe wanapumzishwa, unaweza kuamua wewe mwenyewe kuwa kuku wako aatamie mala ngapi baada ya hapo unampumzisha. Pia kuku wanao atamia inatakiwa chakula na maji viwe kalibu na kiota chake ili asipate usumbufu kufata chakula. Ni vizuri kuwa sehemu salama na tulivu ambayo kuku wengine hawata msumbua au kupasua mayai. Sehemu anapo atamia kuku hakikisha kuwa mvua ikinyeesha hapavuji. Ikitokea kuku wengine umewapa chanjo basi usimsahau na yeye kumpa hiyo chanjo. Kuku anae atamia anahitaji uangalizi mkubwa kwani usipo kuwa makini nae anaweza pata ugonjwa bila wewe kujua, nakuja kufa gafla.

Hizi ni baadhin ya dondoo muhimu kwa mfugaji wa kuku ili kuongeza uzalishaji wa vifaranga.

*Tuungane kutetea maisha ya kuku*

Endelea kufuatilia kwa makala mototo za ufugaji kwenye tovuti hii ya UFUGAJI

 

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!