MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI
Ufugaji wa samaki unamanufaa sana kwa mfugaji kwani unaweza kumuondolea Mtanzania umaskini huku akiendelea kujipatia kitoweo.
Kuna uhaba mkubwa sana wa samaki Tanzania, ukipita katika masoko ya samaki hasa asubuhi utaona wafanyabiashara wanavyogombania samaki. Hii inaonyesha msisitizo kuwa uhitaji wa samaki Tanzania ni mkubwa na watu wengi wanahitajika kuingia katika ufugaji wa samaki. Itawasaidia kujikwamua kimaisha lakini pia kuwafanya Watanzania wengi wapate kitoweo cha samaki.