Na Peter Britz na Samantha Venter
Taarifa kuhusu Africa
Kupanda taratibu kutokea mwanzo kwa ufugaji na uzalishaji wa samaki barani Afrika, inaonyesha kutakuwepo na ukuaji endelevu kwa miongo miwili ijayo. Muingiliano wa fursa za masoko, sababu za kiuchumi na hali ya mazingira ni moja ya vitu vinavyoipa Afrika nafasi ya mbele katika maendeleo ya ufugaji wa samaki.Hii ndiyo mada kuu ya majadiliano
katika mkutano wa wadau wa ufugaji wa viumbe vya majini (World Aquaculture Society) uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini, mwezi Juni 2017.
Rasilmali maji nyingi ambazo hazijatumika, pamoja na ongezeko la uhaba wa samaki, yote haya yanatengeneza fursa ya ufugaji wa samaki kwa ajili ya kukidhi uhitaji wa samaki unaoongezeka kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miji.
Benki ya dunia imetabiri kwamba kufikia mwaka 2030 uhaba wa samaki Afrika utaongezeka na kufika tani milioni 1.8, ikiwa nipamoja na uvuvi uliopitiliza ambao pia utashindwa kukidhi mahitaji. Wakati matumizi ya samaki ya kila mwananchi kupungua kwa ujumla, hii ni kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa samaki kukidhi idadi ya watu inayoongezeka.
Tukiachana na mtazamo wa kihistoria wa ufugaji wa samaki wa kujikimu (ufugaji mdogo), ufugaji wa samaki wa kibiashara umeanza kufanyika katika nchi kadhaa barani Afrika, ukisaidiwa na uchumi wa kisasa katika miji, sekta za kisasa za bidhaa za rejareja na matumizi ya bidhaa zinazozalishwa. Pia ni pamoja na uwekezaji wa serikali za barani Afrika, katika miundombinu na vifaa, kuweka sera zinazosaidia katika ukuaji wa sekta hii ufugaji wa samaki kibiashara.
Pamoja na maono ya baadae ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwamba kutakuwa na kushuka kwa ukuaji wa ufugaji wa samaki kibiashara katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Kutokana na athari za changamoto ya kiuchumi, bei ndogo za bidhaa na ukame, bado kuna misingi ya mahitaji itayosababisha ukuwajiwa ufugaji wa samaki kibiashara unabakia kuwa imara.Wawekezaji na wafanyabiashara mara nyingi hukumbushwa kwamba “Afrika si nchi.” Bara la Afrika lina nchi 53 zenye tofauti kubwa za utamaduni unaosababisha athari katika mila za chakula na ubaguzi wa chakula.Tofauti kubwa ya kiwango cha ukomavu wa uchumi, teknolojia na maendeleo ya viwanda, miundombinu ya biashara, mzunguko wa thamani na huduma mbalimbali na mazingira ya yaliyodhibitiwa; masoko ya kila aina na viwango vya mapato ya ziada na maeneno yenye ardhi ya kila aina.
Hivyo basi, uchambuzi wowote wa shughuli za ufugaji samaki na uwezo wa bara la Afrika haya yanatengeneza fursa ya ufugaji wa samaki kwa ajili ya kukidhi uhitaji wa samaki unaoongezeka kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miji.
SOMA MAELEZO YOTE HAPA