Kutunza chakula cha kuku

Chakula cha kuku ni bidhaa muhimu kutunzwa kwa uangalifu, kwani kisipotunzwa vizuri, na ukawalisha kuku wako:

– Wanaweza kuumwa

– Wanaweza kuacha kutaga

– Au wanaweza kufa

 

SABABU ZA CHAKULA CHA KUKU KUHARIBIKA

 

  1. Wanyama wanaoharibu nafaka

Wanyama kama panya na panya buku ni wajanja na wepesi kujua sehemu unayotunzia chakula, na wakifika wanatoboa mfuko na kula, huku wakiacha chakula kingine kinamwagika. Pia wanyama hawa wanabeba magonjwa ambayo yanaweza yakaathiri chakula na kuku wakila wanadhurika.

 

  1. Wadudu waharibifu

Kuku wanapenda kula wadudu, lakini sio wadudu wote ni safi. Wadudu kama nondo na mende, wanapenda kula chakula cha kuku na kuishi humo. Wadudu hawa wanaweza kubeba magonjwa na kutaathiri chakula, ambapo ukilisha kuku, wanaweza kuumwa au kufa.

 

  1. Fangasi/ukungu

Utunzaji mbaya wa chakula, hupelekea chakula kupata fangasi au ukungu na kuwa mabonge mabonge. Fangasi/ukungu unavyosambaa kwenye chakula, hutengeneza mycotoxins ambayo inaweka sumu kwenye chakula na inaweza kukipa chakula ladha mbaya na kuku hawatakipenda.

 

  1. Unyevunyevu

Changamoto kubwa ya kutunza chakula ni unyevunyevu. Unyevunyevu unahamasisha ukuaji wa fangasi/uvundo. Hakikisha sehemu unayotunzia chakula ni pakavu na kuna hewa ya kutosha, ili kuondoa unyevunyevu.

 

  1. Chakula kilichooza

Chakula cha kuku kilichochanganywa vitu mbalimbali hakidumu milele. Mafuta (mashudu) yanayotumika kwenye kutengeneza chakula cha kuku, baada ya muda huoza, na kufanya chakula chote kioze. Chakula hiki kunakuwa na harufu mbaya na kinakuwa na sumu ambayo itapunguza ukuaji wa kuku. Pia kuku hawatapenda kula chakula hiki, na utaona kuku wako wakipungua uzito siku hadi siku. Ndio maana ni muhimu sana kutunza chakula kwa usahihi.

 

Chakula kitunzwe kwa muda gani?

Chakula cha kuku kitakaa muda mrefu kama kikitunzwa kwenye mazingira makavu na yenye hewa ya kutosha kwa muda wa miezi mitatu hadi sita.

Lakini chakula kitaharibika haraka kama kikipata jua, unyevunyevu, na kuchezewa na wanyama na wadudu waharibifu.

 

Chakula cha kuku kitunzwe sehemu gani?

Weka chakula cha kuku kilichopakiwa kwenye mifuko sehemu kavu yenye ubaridi. Pia chakula kiwekwe juu ya mbao au miti, yaani kisiguse sakafu. Kwani sakafu itakifanya kigande na kuweka uvundo.

 

Muhimu:

Wafanye kuku wako wawe na furaha kwa kuhakikisha chakula chao kinatunzwa sehemu salama, kavu na yenye ubaridi, hivyo hutapata tatizo la chakula kuvunda au kuoza, na kuku wako watakuwa na chakula safi, fresh na watakua haraka na kutaga mayai mengi.

 

Imeandaliwa na

 

Aquinus Poultry Farm

 

0655347932

Leave a Reply