Sungura

Na Rubaba Imani  

UTANGULIZI
Kama mnyama yeyote sungura anahitaji utunzaji mwema ili waweze kuzalisha kwa wingi. Anahitaji kujengewa chumba maalum na kuangaliwa kila siku na kuhakikisha usafi wa vyumba hivi. Na kama watoto wa binadamu pia sungura wanahitaji kupewa chakula kisafi cha hali ya juu kilicho na madini ya protini na kalsham na pia kupewa maji masafi. Kulingana na wazalishaji wa sungura wa Marekani [American rabbit breeders association ARBA] kuna aina 47 tofauti za sungura zinazofungwa kama vile angora,new Zealand white, californian white,French lop,Giant Flemish,dutch,chinchilla rex na nyingine nyingi .
Hapa Tanzania pia kuna aina nyingi zinazo fugwa ambazo ni Angora, Flemish Giant,French lop,Chinchilla, Callifornian white na New Zealand white.

Hapa Tanzania kuna aina zifuatazo

1) New Zealand Whites
Hii ni jamii mojawapo maarufu kwa ufugaji wa sungura wa nyama, na kwa nchi kama Marekani, nyama yake ndiyo bora zaidi kuliko aina nyingine za sungura. Sungura hawa wanaweza kufikisha kilogramu 3.6 hadi 5

2) Californian white Rabbits:
Hawa ni uzao chotara wa sungura jamii ya Chinchilla na New Zealand Whites. Wana manyoya meupe na madoa meusi na wanafahamika kutokana na maumbile yao kama matofali na wanatoa nyama nzuri. Wanaweza kufikisha kilogramu kati ya 3.2 hadi 4.8.

3) American Chinchilla:
Hawa ni aina bora ya sungura kwa ajili ya nyama na wanarandana na sungura jamii ya Chinchilla ambao hata hivyo ni wakubwa kwa maumbo. Wana rangi ya kijivu na nyama yao inaweza kufikisha hadi kilogramu 3.6. Nyama yake inapendelewa Zaidi kukaangwa ama kubanikwa.


4) Silver Foxes:
Hawa ni sungura rafiki zaidi kufugwa majumbani ambao wanafaa kwa mapambo pamoja na nyama. Aina hii ni adimu sana na wanaweza kufikisha kilogramu kati ya 4 hadi 5. Wana rangi ya fedha yenye kivuli cheusi na masikio yeliyoinuka, kama alivyo mbweha wa rangi ya fedha.


5) Champagne D Argent:
Aina hii ya sungura wa kihistoria anayevutia imetumiwa kwa nyama tangu mwaka 1631. Nyama yao inapendwa ulimwenguni kote na ni wazuri kwa kufugwa. Unaweza kuwakuta katika rangi mbalimbali kama nyeupe, rangi ya maziwa au chocolate.
Hizo tu nia aina za sungura ambazo nizuri katika ufugaji ambazo ni za kisasa zenye kutoa faida ya hali ya juu nyingine tutaendelea kukuletea kadri somo la sungura linavyo eleza.

KUPANDISHWA
Sungura anatakiwa kupandishwa anapokuwa na umri wa miezi mitano mpaka sita. Na sungura dume anapanda napokuwa na umri kati ya miezi saba.Sungura jike anatakiwa kukaa na dume kwa dakika 30 tu kisha kuondolewa katika banda.sungura anabeba mimba kwa muda siku 28-32 mpaka kuzaa(gestation period).
Kwa kawaida sungura anapokuwa na mimba anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha ili kumsaidia kutengeneza maziwa ya kutosha pindi atakapo kuwa amezaa watoto wanyonye vizuri. Siku tatu mpaka nne kabla ya kuzaa unatakiwa kumwandalia sungura mazingira ya kuzalia kwa kutandaza majani makavu au maranda katika banda lake.wakati mwingine sungura anaweza akashindwa kuzaa mwenyewe ni vyema mtu alie karibu nae kumsaidia
Watoo wa sungura wanazaliwa bila manyoya na macho yaliyo funga. Manyoya yanaanza kukua taratibu baada ya siku chache na macho yanaanza kufunguka baada ya siku kumi.katika kipindi hiki mfugaji anashauriwa kuwa karibu na sungura muda wote kwani wanaweza kupata tatizo lolote
Sungura anaweza kuzaa watoto 2-14 na wanahitaji kunyonya angalau miezi miwili kabla ya kuachishwa.unaweza kumpunguzia pia sungura watoto wa kunyonyesha kwa kuwapeleka kwa sungura mwingine aliye zaa watoto wachache cha msingi ni kuwazoesha watoto harufu ya sungura asiye kuwa mama yao . hii inamsaidia sungura mwenye watoto wengi kupunguza maumivu ya kunyonyesha.

KUACHISHA WATOTO
Sungura watenganishwe banda na mama yao baada ya miezi mitatu na wakati huo mama yuko tayari kurudishwa kwa dume kwaajili ya kupandwa na baada ya miezi minne sungura waliozaliwa watenganishwe jike na dume ili kuzuia kuzaliana ndugu. Sungura jike apandishwe mara nne kwa mwaka ili kumpa afya nzuri na nguvu ya kuzaa watoto wenye afya.

CHAKULA CHA SUNGURA
Sungura wanahitaji chakula chenye protini mafuta,vitamin,madini na chakula chenye kuupa mwili nguvu
Pia unaweza kuwalisha sungura kwa kuwapatia vyakula kama
1. Majani ya mimea na mimea wayoipendelea,nyasi,magugumajani ya viazi vitamu pia mbogamboga kama cabbage na sukuma wiki
2. Mazao yenye mizizi kama karoti viazi vitamu na mihogo
3. Majani makavu
4. Mazao kama mahindi,ngano na mtama
5. Vyakula vyenya protini kama mashudu ya soya
6. Pia unaweza kuwapatia chakula cha kuku (grower mash)kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho.
tumia mabakuli ya kigae,plastiki au jengea kwa saruji maji ya kunywa sungura na yabadilishwe kila siku

MAGONJWA YANAYOWASUMBUA SUNGURA JINSI YA KUYAEPUKA NA TIBA
Kutambua sungura mwenye afya na mgonjwa
i. Ngozi yake inatakiwa kuwa nyororo na yenye mng’aro
ii. Awe na hamu ya chakula
iii. Kula kwake na umezaji wake uwe wa kawaida
iv. Kujisaidia kwake kuwe kwa kawaida kwa kiwango sahihi na kinyesi kiwe na mwonekano sahihi
v. Macho ya sungura yawe mang’avu na yasitoe machozi
vi. Atembee kiurahisi kwa uhuru na upumuaji uwe wa kawaida na wa kimya
vii. Uzito na ukuaji wasungura mkubwa hautakiwi kuongezeka
viii. Ulaji na utafunaji wa sungura unatakiwa uwe wa kawaida
ix. Joto la kawaida kwa sugura ni 39c
x. Kama sungura anatokwa majimaji katika pua,machoni,mdomoni ,machoni kwenye maziwa ama sehemu za haja kubwa ni dalili ya ugonjwa
xi. Miguu ya sungura si sawa na wanyama wengine nyayo zao zimefunikwa na manyoya angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo
xii. Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia sungura usumbufu wakati wa kula waone waataam kwani yahnahitaji kupunguzwa dalili kuu ni sungura kushindwa kula ndani ya masaa 12
xiii. Mwili wake unatakiwa kuwa imara kama anaonekana kuzubaa na kupooza ni dalili ya ugonjwa
Kuzuia magonjwa/kuepuka magonjwa
Katika banda linalotunzwa vizuri hakuna magonjwa ya mara kwa mara.Unatakiwa kuzuia
MAGONJWA
Kuna magonjwa mawili tu makuu yanasumbua sana sungura ambayo ni:

COCCIDIOSIS [ MAGONJWA YA KUHARA]
Ugonjwa huu unaathiri zaidi sungura wadogo
Dalili
Kuharisha ambako wakati mwingine kinyesi kinaweza kuwa na rangi nyeupe au kuwa na chembechembe za damu,Mnyama kukosa hamu ya kula na mnyama anaweza kufa endapo atacheleweshewa matibabu.
Kwa sungura mwenye mimba anapokuwa ameaathirika sana na ugonjwa huu anaweza kuwaambukiza watoto walio tumboni na hali hii inasababisha ugonjwa huu kuingia kwenye maini ya watoto moja kwa moja
Ugonjwa huu unatiba kwa dawa zote zinafahamika kama Coccidiostants unawawekea katika maji ya kunywa na chakula pia ni vizuri kuwa tenga wanyama wangonjwa na wazima na kuwatenga wanyama wageni wanaingizwa na wenyeji angalau kwa muda wa wiki mbili ili kugundua kirahisi magonjwa na kuzuia kuambukizana.

UKURUTU [ EAR CANCER/ MANGE]
Ugonjwa huu unasababishwa na utitiri na viroboto na unaathiri sehemu za ndani za masikio ya sungura.Ugonjwa siyo mkubwa sana lakini unamsumbua sana mnyama
Dalili
Mnyama nakua anatikisa kichwa mda wote na kuchezesha masikio kutokana na muwasho anaoupata
Mnyama anavimba vitu vidogovidogo kama upele sehemu za ndani na nje ya masikio na endapo kuvimba kutazidi sana kunaweza kufanya masikio yakalala na siyo kuwa wima
Zuia kwa kuzuia panya kuingia katika banda kwani panya ndio wanaleta viroboto kwa wanyama pia nyunyizia dawa za wadudu kama akheri powder kwenye mabanda yao ili kuzuia viroboto.
Magonjwa mengine ni kama
Pneumoni: hii inatoke sana kipindi cha baridi na katika mabanda yasiyo na hewa ya kutosha
Gastro:haya ni maumivu ya ndani na yanasababishwa sana na chakula anacho kula mnyama
Internal Parasite: minyoo kama Ascaris wanaotokana na kula majani.
Hivyo chanjo ya minyoo kama piperazine angalau kila baada ya miezi mitatu kwa wanyama inashauriwa kuzingatiwa.Pia ni muhimu kuepuka kuwarisha wanyama majani yaliyo kandokando ya barabara.

BANDA LA SUNGURA
Kuna aina mbili za mabanda ya sungura,kwanza ni yale ya kuwafungia ndani mda wote bila kutoka nje na pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje katika ua maalumu.Katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuwaruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura na pia wanaleta viroboto kwa sungura.

UFUGAJI WA NDANI
1. Usitumie banda la kioo(aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2. Sakafu ya vyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura kwani wakiumia ni mpaka wapone wenyewe au mchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake hivyo siku ukimchinja atabaki na dawa hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3. Ukubwa wa banda usipungue mita 4*2 kwa kila sungura
4. Chini kuwekwe matandazio ya nyasi ama maranda ya mbao,lakini maranda yatokanayo na miti yenye mafuta kama mikaratusi hayafai,wawekee blanket au kipande cha taulo kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi,
5. Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha wakati wanapohisi hatari unaweza kutumia box gumu,mbao au plastiki.

UFUGAJI WA NJE
1. Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku(wire mesh) kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka,mbwa,mwewe nk
2. Upande mmoja uwe na mabanda,sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwaajili ya sungura kupumzika
3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuzuia wadudu au mbolea pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu
Kwa ujula banda linatakiwa kuwa na haya yafuatayo kwa sehemu zote yaani ufugaji wa ndani na ule wa nje
1. Liwalinde sungura dhidi ya maadui
2. Liwe na miundombinu mizuri itayo rahisisha kutunzwa kwa kufanyiwa usafi
3. Banda linatakiwa kupitisha hewa na mwanga wa kutosha ili kuwasaidia sungura kupumua vizuri
4. Banda liezekwe ili kuwakinga sungura dhidi ya jua na mvua

FAIDA ZA UFUGAJI WA SUNGURA
1. Kujipatia kitoweo
2. Kujiongezea kipato kwa kuuza
3. Kujiajiri mwenyewe
4. Kukuza uchumi wa nchi
5. Unajipatia mbolea ya samadi
6. Hawana gharama katika kuwatunza kama wanyama wengine

HASARA ZA UFUGAJI WA SUNGURA
Hakuna hasara katika ufugaji wa sungura zaidi ni changamoto tu unazokutana nazo katika kuwatunza kama usipokuwa makini inaweza kuwa hasara changamoto hizo ni kama vile:
1. Sungura kutoroka kwa njia ya kuchimba mashimo
2. Kukosa chakula cha kutosha kuwalisha hasa wakati wa kiangazi
3. Sungura kuugua hata kufa hasa unaposhindwa kuwahumia vizuri kuanzia usafi wa banda hata chakula na maji unayowapatia
4. Kukosa soko kutoka na watu kutojua faida za ulaji wa sungura

NB: usafi wa banda ufanyike kila siku ili kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika na kinyesi kilichoganda fagia na badili matandazio anaglau mara moja kwa wiki manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto.

MUHIMU
Usimbebe sungura kwa masikio yake huwa wanaumia sana shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba.

 

Leave a Reply