Mwongozo wa ufugaji wa samaki aina ya sato

FUGA SAMAKI KWA KIPATO ENDELEVU NA CHAKULA BORA

UTANGULIZI

Ufugaji wa samaki unafaida zifuatazo: huongeza kipato kwa wakulima, hurahisisha upatikanaji wa chakula hasa chakula aina ya protini,unapunguza kasi kubwa ya uvunaji wa samaki katika mazingira ya asili kama mito bahari na maziwa na pia ufugaji wa sato ni chanzo cha ajira. Sato ameonekana kua  samaki anaefanya vizuri kwa kufugwa katika nchi nyingi za Africa, kwa sababu ana uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira magumu na hukua kwa kasi kwa muda mfupi, hufikia kiasi kinachohitajika sokoni, pia sato wanauwezo wa kuzaliana kwa urahisi na kwa wingi sana hasa wakiwa wanapewa chakula kizuri.Katika mazingira ya asili, sato hula vyakula vya aina mbalimbali,vinavyoweza kuwa vimelea vya majini (mimea midogo midogo inayoota majini) na wanyama wadogo wadogo wanao ishi majini mfano minyoo. Katika bwawa mimea midogo midogo inayoota majini inaweza kukuzwa kwa kurutubisha bwawa na mbolea itokanao na viumbe hai kama vile kuku, mbuzi au mimea (miti) pia mbolea ya viwandani.Wakati sato wanatafuta chakula hutumia nishati kubwa sana ili kukamilisha mahitaji yao ya mwili wakiwa katika mazingira ya asili. Zaidi wakiwa katika hali ya ufugwaji samaki wengi hupatika kwenye eneo dogo, matokeo yake huwa nivigumu na hasara kuendelea kutegemea chakula cha asili. Hivyo huwa inalazimisha kutengenza na kulisha chakula cha viwandani, kinacho tengenezwa kwa kufuata sayansi ya mnyama na hali aliyo nayo wakati huo, ili kutoa faida endelevu kwa mkulima wa samaki.

Ulishaji wa vyakula vya viwandani vinamuwezesha mkulima kupata faida kulingana na ubora wa chakula anacho wapa samaki, kwani vyakula vya kutengeneza (viwandani) hutengenezwa vikiwa na virutubisho vinavyo hitajika kwa samaki wenye lika husika au hali furani waliyonayo samaki kwa wakati huo, mkulima anaweza kulisha samaki chakula kulingana na mahitaji ya samaki kwa wakati huo, hii hupelekea uzalishaji wenye tija kwa mkulima. Hii ni muhimu ukifikiria kuwa gharama za chakula huchukua 60-70% ya gharama zote za ufugaji wa samaki.

 

Uwezo wa chakula cha samaki kufanya kazi unategemea zaidi;

1.Uwezo wake wa kukizi virutubisho vinavyo hitajika kwa samaki wanaokua.

  1. Uwezekano wa kuliwa na samaki
  2. Uimala wake katika maji na matokeo yake kwenye ubora wa maji.

Kuhakikisha matokeo mazuri kutoka chakula kamili (punje zilizotengenezwa) hatua zifuatazo lazima zifuatwe kabla na wakati wa uzalishaji.

 

Hatua za mwanzo

Uandaaji wa bwawa

  • Hakikisha bwawa halivuji.
  • Hakikisha bomba linaloingiza maji kwenye bwawa limewekewa wavu ili kuzuia wadudu kuingia bwawani, mfano chura na kaa.
  • Hakikisha bwawa limerutubishwa kama inavyo shauriwa na wataalamu

Jaza maji kwenye bwawa.

Jaza maji kwenye bwawa lilo fungwa wavu kwenye bomba linalo ingiza maji.

Hakikisha kina ni wastani unaoshauriwa na wataalamu wa ufugaji wa samaki ambao ni 1M (cm 80 kueleke bomba la kuingizia maji na siyo zaid ya mita1.2 kuelekea bomba la kutolea maji).

 

Upandikizaji wa vifaranga vya samaki

  • Pandikiza vifaranga vya samaki ndani ya siku 10 baada ya kujaza maji kwenye bwawa pia wakati utakapoona maji ndani ya bwawa yana ubora unaotakiwa (kijani cha kutosha). Hii itazuia uwezekano wa mayai ya chura kutawala bwawa kwa kufanya mushindano mkali kwa chakula kati ya samaki na chura.
  • Pandikiza vifaranga vya samaki vyenye umri sawa.
  • Kiwango cha chini cha kupandikiza katika bwawa la kukuzia samaki ni gramu 7 kwa kila kifaranga.vifaranga vya samaki chini ya gramu 7 vinatakiwa kuwekwa kwenye bwawa la kulelea watoto wa samaki ili wakue kufikia gramu 7 au 10, tayari kupandikizwa kwenye bwawa la kukuzia samaki ili kufikia kiwango cha soko.
  • Ni vizuri kupandikiza vifaranga madume tu kwa kuwa yana kuwa haraka sana kuliko majike ambayo huzaliana kwa wingi na kukua taratibu sana.
  • Idadi ya kupandikiza: Inategemea na uwezo wa bwawa kuhifadhi samaki mpaka muda wa kuvuna pia malengo ya kiwango cha uvunaji. Uwezo wa bwawa kuhifadhi samaki aina ya sato ni kilo moja (1) kwa kila mita moja ya eneo kwa bwawa lililo rutubishwa vizuri. Kama samaki aina ya sato watapandikizwa kwa wingi,kasi ya ukuaji huwa ndogo sana. Chini ni mingi ya upandikizaji wa samaki aina ya sato

 

Uangalizi wa bwawa

  • Weka chujio kwenye bomba la kuingizia na kutoa maji kwenye bwawa wakati wote wa mzunguko wa uzalisha wa samaki.
  • Usiruhusu maji kuingia na kutoka bwawani wakati wote. Ongeza maji tu kujazilizia kiasi kinacho takiwa bwawani au pale ubora wa maji unapopungua au kuharibika kabisa.
  • Rutubisha bwawa kila wiki kuhakikisha kuwa maji ni ya kijani kinacho shauriwa na wataalamu wa ufugaji wa samaki.
  • Hakikisha kina cha maji hakizidi sentimita 100 au mita moja na hakipungui sentimita sabini (70)

 

Vipimo vingine

  • Usilowanishe chakula cha samaki kabla ya kulisha samaki.
  • Hifadhi chakula cha samaki mahali ambapo pana joto la wastani kati ya nyuzi joto 25-30, na iwe mbali na mwanga wa jua ule wa moja kwa moja.
  • Vuna samaki kabla ya bwawa kufikia hali ambayo itazuia ukuaji wa samaki, hii itamuwezesha mkulima kupata faida na kuwa na ufugaji wa samaki endelevu.

 

NAMNA YA KULISHA CHAKULA KINACHO ELEA

  • Kumbuka jedwali la kulishia samaki aina ya sato kama msingi wako wa ulishaji samaki.
  • Tumia aina na ukubwa sahihi wa chakula kulingana na ukubwa wa samaki unaowafuga.
  • Lisha kiasi sahihi cha chakula. Kiasi cha chakula ambacho samaki anahitaji kulishwa kinategemeana na uzito wa mwili wake pia ubora wa maji na afya ya samaki kwa wakati huo.
  • Lisha samaki mara idadi sahihi kwa siku. Jedwali la ulishaji samaki aina ya sato lina onesha idadi ya ulishaji samaki kwa siku, samaki wenye ukubwa sawa walishe wakiwa kenye bwawa moja.
  • Lisha kwa muhemuko.Lisha kulingana na muhemuko wa samaki kwenye chakula kwa wakati huo, kama samaki hawata onesha muhemuko kwenye chakula, usiongeze chakula kingine kwa wakati huo.
  • Rekebisha ulishaji kulingana na uzito halisi walionao samaki wako.
  • Weka kumbukumbu ya kiasi cha chakula ulicho walisha samaki wako, ili kusaidia kujua kiwango cha ukuaji wa samaki na ubora au umakini wa mlishaji wakati wa uzalishaji.
  • Kama unafuatilia misingi yote, mpaka muda wa uvunaji, mkulima atakuwa anatumia kiasi cha kilo moja na nusu (kilo1.5) ya chakula kuzalisha kilo moja (1) ya samaki aina ya sato.Kiasi cha chakula kinacho tumika kuzalisha au kutoa kilo moja ya samaki ni muhimu kukijua kwa mkulima wa samaki, kwani kina msaidia kujua kama amepata faida au laa.

 

Namna ya kuwafundisha samaki kula kwa mwitikio au muhemuko.

  • Kulisha kwa mwitikio, samaki wanahitaji kufundishwa kula kwa mwitikio katika sehemu moja ya uso wa maji ya bwawa au mfereji wa maji.
  • Ita samaki waje kula katika sehemu moja iliyoandaliwa vizuri wakati wote unapotaka kuwalisha. Mfano kwa kutoa sauti ya muruzi au kugonga ardhi au ukuta wa bwawa kabla ya kuwalisha samaki wako.
  • Jaza chakula cha samaki kwenye mkono halafu kitupie bwawani subili kwa dakika chache, kuona kama watakuja kula. Wakija kula ongeza chakula. Kama hawatakuja usiongeze chakula hata kidogo.
  • Siku inayofuata, fanya vilevile mpaka samaki wata zoea kula kwa mwitikio, kwa siku zamwanzo wengine wata chelewa kufika mahali pachakula, watakuta kimeisha.Hii inaweza kuchukua siku kazaa (4-6 siku).
  • Wiki ya kwanza, usiwape chakula kingi zaidi ya kile kilicho oneshwa kwenye jedwali la kulishia samaki.
  • Usirushie chakula kwenye bwawa taratibu. Tumia chombo maalumu kutawanya chakula bwawani.
  • Samaki wanatakiwa kumaliza chakula walichopewa ndani ya dakika 15 Kama hawatamaliza chakula, punguza kiasi. Kama watamaliza chakula chote chini ya dakika 5, ongeza chakula kiasi ambacho utaona wametosheka.
  • Tunza kumbukumbu ya chakula walichokula samaki kwa siku. Utunzaji wa kumbukumbu unahitaji kuwa endelevu, kwa faida ya mkulima mwenyewe.

 

KUMBUKA;

  • Lisha chakula chenye 25% ya protini tu pale ambapo bwawa limerutubishwa vya kutosha (maji ya kijani).
  • Kama bwawa halijarutubishwa vya kutosha (maji siyo ya kijani), endelea kulisha chakula chenye 30% ya protini.
  • Vifaranga vya sato vinapatikana kwa urahisi ukilinganisha na kambale, vifaranga vya sato vizuri ni vile vinavyo patikana kwa kuzalishwa kwenye vitalu (hatchary),kwa kunyang’anya mayai kwenye mdomo wa sato jike kisha yana atamizwa kwenye vifaa maalumu au kwa njia ya kuweka majike manne na dume moja (4:1) kwa kila mita moja ya eneo ya bwawa au tenki ya kufugia samaki.Wazazi walio wekwa kwa uwiano nne kwa moja kwa kila mita moja ya eneo wanapaswa kulishwa chakula kamili chenye protini ya asilimia 35 ili waweze kuzaa vizuri na kuwa na afya nzuri na walishwe mara mbili kwa siku. Njia hizi mbili ni nzuri kwani hutoa vifaranga wenye umri sawa na uzito unaokaribiana,kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kufuga samaki anashauriwa kutafuta vifaranga walio zalishwa kwa njia moja wapo kati ya hizi mbili zinzoshauriwa na wataalamu wa ufugaji wa samaki.
  • Kitabu hiki kimejibu maswali mengi yanayo watatiza wafugaji wa samaki pia wanafunzi wanaosoma ufugaji wa samaki hapa nchini. Kitabu hiki kinajumuisha maswali yote muhimu ya ufugaji wa samaki yaliyokuwa yakiulizwa na wafugaji au wanafunzi wakati wa nanenane kanda ya mashariki mwaka 2013.

 

Kifaa cha kuongezea hewa katika

 

Tank za kufugia samaki pamoja na kuzalishia vifaranga

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply