Ufugaji wa kuku bora wa nyama (broiler) hatua kwa hatua

Pakua App ya Tovuti hii HAPA

 

Na Mwandishi wetu: Sefania Kajange

Lengo la somo hili ni kukuwezesha wewe mfugaji kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi na kukuwezesha wewe kupata faida kwa muda unaokusudiwa.

 

Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

 

Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba/ mahali unapotaka kufugia ni kama inavyoonyesha hapa chini.

 

 1. Mazingira yanayolizunguka banda la kuku na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.

 

 1. Hakikisha sehemu ya kulelea vifaranga (brooding area) inawekewa chanzo cha joto saa moja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya eneo la kulelea vifaranga.

 

 1. Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga wafikishe kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe glucose na baada ya hapo chakula.

 

 1. Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye kiticha gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka msongo (stress).

 

 1. Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10 chicks/1m square) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

 

Mambo ya kuzingatia baada tu ya vifaranga kufika shambani mwako

 

 1. Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye boksi mara moja. Unapowachelewesha ndani ya boksi utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.

 

 1. Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa 23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.

 

 1. Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamini kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.

 

 1. Hakikisha unapanga vyema vyombo vya chalula (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

 

JOTO

 

 1. Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na chanzo cha joto.

 

 1. Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya nyuzi joto 40-41. Njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo yako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto.

 

 1. Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

 

Ratiba ya mwanga

 

Umri wa kifaranga (siku) ………………….Masaa ya giza

0-7 ————————————————–>0

8-21————————————————->3

22 —————————————————>4

23 —————————————————>5

24 —————————————————>6

5 Siku kabla ya kuuza ————————->5

4 Siku kabla ya kuuza ————————-> 4

3 Siku kabla ya kuuza ————————->3

2 Siku kabla ya kuuza ————————->2

1 Siku kabla ya kuuza ————————->1

 

Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35

 

MAJI

Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihabarishi mojawapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. Kuku kutokunywa maji ni kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida.

 

Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 (vyombo vya maji) kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

 

CHAKULA

Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia au magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula kwenye vyombo maalumu vya kulishia kuku (feeders).

 

Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja, na hii inafaa itoshe eneo la asilimia 50 tu katika eneo la kulelea vifaranga (brooder).

 

Kwa feeder za kawaida inashauriwa/ inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, maji

 

maji na panya.

 

Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi.

 

Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa 8 kisha masaa 24 kama wamekula na hii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume cha hapo inaonyesha hawajala.

 

AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

 

Chakula cha vifaranga (Super starter)

Vifaranga wapewe kilo 0.5 ya chakula kwa kila kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa vidonge (pellet) kwa muda wa wiki 2 au unaweza kufuata mfumo wa kawaida wa ulishaji.

 

Chakula cha kuku wanaokua (Grower)

 

Kuku nwanaokua wapewe kilo 1.5 ya chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa vidonge (pellet) kwa muda wa wiki 2 au unaweza kufuata ratio ya mfumo wa kawaida au bila kuwapimia.

 

Kuku wakubwa (Finisher)

Kuku wa hatua hii wapewe kilo 1.5 ya chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza na hapo unaweza kuwauza siku yoyote.

 

 

MAMBO MUHIMU KWA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA KULINGANA NA UMRI WAO

 

MFUMO WA KWANZA

 

SIKU 1-5

 

Wapewe glucose na mchanganyo mmojawapo kati ya hii ifuatayo;

 • Neoxyvital au OTC plus na typhorium au trimazine
 • Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

 

CHAKULA

 

 • Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

 

SIKU YA 6

 • Vitamini (vitastress)

 

SIKU YA 7

 • Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

 

WIKI YA PILI

 • Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

 

WIKI YA TATU

 • Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

 

WIKI YA NNE

 • Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

 

WIKI YA TANO

 • Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

 

WIKI YA SITA

 • Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni
 • Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo

 

 

MFUMO WA PILI

Ni huu wa kawaida ambao ni kufuata ratiba ya kawaida. Lakini inatakiwa tu kuwa makini

Na huu mfumo kila mtu anaufahamu kama hivi.

 

Broiler huwa wana aina mbili za ulishaji.

 

1 Kuanza (supper starter) na kumaliza (finishers)

 1. Kuanza (starter), kukuza (growers) na kumalizia (finishers)

 

Kwanza:

Aina ya kwanza huwa ni wiki 2 za mwanzo hupewa chakula cha kuanzia (Supper starter) na wiki mbili zinazofuata mpaka kuuzwa hupewa chakula cha kumalizia (broiler finishers)

 

 

Pili.

Aina ya pili huwa chakula cha kuanzia wiki 2 za mwanzo (supper starter) chakula cha kukuzia (broiler growers) wiki ya 3 na chakula cha kumalizia (broiler finishers) wiki ya 4 hadi kuuzwa

 

🙏🇹🇿✍

Fuga KIBIASHARA kwa MALENGO timiza NDOTO yako

Kuwasiliana na mwandishi wa makala hii! 0718973860

Leave a Reply