Ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua: utangulizi

Na Augustino Chengula

UTANGULIZI

Ufugaji wa kuku wa mayai katika Makala hii ya ufugaji wa hatua kwa hatua nitaelezea ufugaji wa kuku wa mayai kwa lengo la uzalishaji wa mayai kibiashara. Nimelenga ufugaji utakaomtoa mfugaji kutoa hatua moja kwenda nyingine na si ufugaji wa mazoea. Kuku wa mayai ni kuku maalumu kwa ajili ya utagaji wa mayai na uleaji wake unapaswa uangaliwe kwa umakini tangu kifaranga kikiwa na siku moja na kuendelea hadi kuku anapofikia umri wa kuanza kutaga mayai na kuendelea. Ufugaji wa kuku wa mayai umegawanyika katika hatua tano kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Hatua hizi zimepangwa kwa kuangalia (1) ukuaji (2) Mahitaji ya nafasi kwenye nyumba na (3) Aina ya chakula anachotakiwa kupewa.

Hatua Umri
Kinda/Kifaranga Siku1 hadi wiki 6
Umri wa ukuaji Wiki 6 hadi 12
Tembe/Wanaokaribia kutaga Wiki 12 hadi 20
Wanaotaga Wiki ya 20 hadi 120
Ubadilishaji wa kuku wazee Kuanzia wiki ya 80 na kuendelea

 

Kwa kawaida kuku wa mayai huanza kutaga mayai wakifikisha wiki 18 hadi 20 na wataendelea kutaga mfululizo hadi watakapofikisha wiki ya 72 hadi 78. Wachache watafika wiki 120 kama inavyoonyeshwa kwenye jwadwali hapo juu. Katika mfuatano wa Makala hizi nitaelezea hatua zote za ukuaji wa kuku wa mayai na nini cha kufanya kwa kila hatua ili uweze kupata uzalishaji unaotegemewa kwa kuku wako.

 

Endelea kufuatilia makala hizi za ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua na katika hatua ya kwanza itakayokujia hivi karibuni itahusu Maandalizi ya awali ya ufugaji wa kuku wa mayai. Itakuelewesha nini cha kufanya katika hatua za mwanzo za mradi wako wa ufugaji wa kuku wa mayai. Karibu Fuga Kibiashara.

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!