Ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua: utangulizi

Utunzaji wa kuku wa mayai walio katika umri wa ukuaji (Wiki ya 6 au 8-12)

Hii ni hatua ya kati ya ukuaji wa kuku wa mayai, si vifaranga tena bali ni kuku wa mayai walio katika hatua ya kati ya ukuaji. Umri wa ukuaji kwa kuku ni hatua ya kwanza muhimu hasa kwa wanaotumia vizimba au kinengunengu kulelea vifaranga na mifumo mingine ya aina hiyo. Wakati huu mahitaji yao pia yanabadilika kutoka ya vifaranga kwenda ya kuku anayekua. Umri huu wa kati huwa kati ya wiki 6 au 8-12 ambapo kuku wanapofikisha umri huu lazima waondolewe kwenye vifaa vya kuwalelea na kuwahamishia kwenye maeneo makubwa kiasi yanayoendana na ukuaji wao.

Nyumba yao itandazwe malanda ya mbao au pumba ya mpunga ili waweze kuishi kwa furaha. Haishauriwi kuwaweka kuku wakati huu kwenye vizimba. Katika hatua hii chakula (growers mash), maji na baadhi ya chanjo muhimu (chanjo ya mdondo/kideri, Gumboro, Tyfoidi, Ndui na Kipindupindu) ni muhimu wakapewa kwa kufuata utaratibu. Mchanganyiko wa vitamin mbalimbali wanaweza kupewa wakati huu ili kuwaongezea kinga dhidi ya magonjwa. Hakikisha unaosha vyombo vya chakula na maji vilivyotumika kila siku kupunguza maambukizi ya magonjwa. Kuku wapewe mwanga angalau kwa masaa 12 kwa siku pamoja na hewa.

Kama hukukata midomo katika hatua ya vifaranga (kuanzia wiki ya pili) unaweza kukata midomo katika hatua hii ili kuwafanya kuku wasidonoane na kupunguza uwezekano wa kudonoa mayai wakifikisha umri wa kutaga. Kama unapanga kufuga kuku wa mayai kwenye vizimba basi ukataji wa midomo hauhitajiki.

Katika hatua hii kuku wasiokua vizuri, wenye dalili za magonjwa ni vema wakaondolewa mapema iwezekanavyo. Vifo kutoka umri wa vifanga hadi ukuaji inatakiwa isizidi aslimia 5, vinapozidi basi kunakuwa na tatizo linalotakiwa kuchukulia hatua za haraka.

KUMBUKA: 1. Usiongeze urefu wa mchana katika hatua ya ukuaji (wiki 8-14).

  1. Usiongeze urefu wa mchana wakati wastani wa kuku wako ni chini ya gram 1250).
  2. Vifo tangu hatua ya vifaranga hadi ya ukuaji isizidi asilimia 25

Leave a Reply