Na Dua Ramadhan

Minyoo (Red Worms) ni chakula kizuri sana cha kuku, Bata na Samaki kwani minyoo wanaprotini nyingi sana, kuku, wakipewa minyoo wanakuwa kwa haraka na kuwafanya kuwa na maumbile makubwa sana (wanakuwa na uzito mkubwa).

Kutengeneza minyoo ya chakula (Red worms planning) Red Worms planning ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki. Zipo hybrid Red Worms ambazo mara nyingi hununua sample kutoka nje ya nchi kama kenya, China na hapa Tz.

Fuata hatua zifuatazo kuzalisha red worms

  1. Chukua mavi ya ng’ombe mapya au ng’ombe aliyechinjwa mavi ya tumboni
  2. Kusanya damu damu,ngozi, utumbo,magoroto,nyamanyama n.k
  3. Pakia kwenye kiloba au gunia
  4. Chimba shimo la wastani kisha mwagia maji ndoo kubwa 4 au 5
  5. Fukia hilo gunia na mwaga maji ndoo 2 au 3 kubwa, Mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 6.
  6. Baada ya siku hizo kupita fukua na chepe, utakuta minyoo mitupu ya kutosha kwa ajili ya chakula cha kuku, bata na samaki.na siku zinavyozidi kwenda ndo wanazidi kuzaliana na kuwa wengi na wakubwa. Utakuwa unawezo wa kuvuna ndoo 1 kubwa kila baada ya wiki moja, utakuwa unavuna kwa muda wa miezi 2 na nusu, na unaweza ukazalisha tena upya.

Kumbuka kuwa hii itakusaidia kupunguza gharama ya kununua chakula cha kuku na pia kuku wako kuwa na uzito mkubwa sana

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!