Ujenzi wa banda la kukuPUjenzi wa banda la kuku

Kuku wanahitaji kujengewa banda ili wasiathiriwe na madhara mbali mbali kama wanyama wakali, wezi na mabadiliko ya hali ya hewa. Vile vile banda bora hurahisisha kazi ya utunzaji.

Mahali pa Kujenga Banda
Sehemu nzuri ya kujenga banda ni:
– Ile inayofikika kwa urahisi
– Ile yenye mwanga wa kutosha
– Isiyo na upepo mkali
– Isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.

Sifa za Banda Bora
Sakafu:
-Sakafu inaweza kuwa ya saruji, mbao au iliyosiribwa kwa udongo. Sakafu iliyojengwa kwa saruji ni imara na bora zaidi.
– Isipitishe unyevu, isiwe na nyufa na iwe rahisi kusafishwa.
Ukuta
Ukuta ni lazima uwe imara ili uweze kushikilia paa. Ukuta unaofaa ni wa matofali ya saruji au ya kuchoma. Kama hayapatikani, unaweza kutumia matofali mabichi, udongo, miti, fito, mabanzi au mabati. Ikiwa ni ukuta wa mabanzi au fito ni muhimu kuondoa magamba na kupaka dawa ili kuzuia mchwa.
Katika sehemu za joto, ukuta ujengwe mita moja kutoka chini kwenda juu na sehemu iliyobaki izibwe kwa kutu’mia wavu ili kuingiza hewa na kuzuia wanyama wakali. Sehemu za baridi ukuta ujengwe kutoka chini kwenda juu ili mradi kuwe na madirisha ya kutosha ya kupitisha hewa. Ni muhimu kusiriba ukuta ili kuzuia nyufa. Vile vile inarahisisha kusafisha na kunyunvizia dawa za kuzuia wadudu.
Paa
Liwe imara na lisilovuja.
Liezekwe kwa kutumia mabati, nyasi, madebe, makuti au vigae.
Vipimo njia banda
Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea na umri, aina na njia ya ufugaji.
Kwa muda wa majuma manne ya mwanzo eneo la mita mraba 1 au eneo la hatua moja linatosheleza vifaranga 16. Banda lenye eneo la mita mraba 16 linaweza kulea vifaranga 320 hadi majuma 4. Baada ya majuma manne ya umri,nafasi iongezwe, hii itategemea na aina ya kuku na njia itakayotumika katika ufugaji kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali namba 1.

Jedwali Na. 1
Idadi ya Kuku katika Eneo la Mita mraba 1 Kufuatana na Aina na Njia tofauti za Ufugaji.

Aina ya Kuku
Njia za Ufugaji Kuku wa Mayai Kuku wa Nyama
Sakafu ya matandazo 3 – 4 6 – 8
Ufugaji wa kwenye vichanja maalumu vya chuma 8 – 12 15 – 25

 

Banda lenye eneo la mita mraba ishirini linatusha kuku wa mayai 60 hadi 80: au kuku wa nyama 120 hadi 160.

 
Plani ya nyumba ya kuku 80 wa kutaga mayai au 160 wa nyama (kwa ubavuni).

 

 
Plani ya nyumba ya kuku 80 wa kutaga mayai au 160 wa nyama (kwa juu).

 

 
Plani ya nyumbaya kuku 500 wa kutaga mayai au 1000 wa nyama (kwa juu). Kila chumba kinatosheleza kuku 125 wa kutaga mayai au 250 wa nyama.


Plani ya nyumbu kuku 500 wu kutaga mayai au 1000 wa nyama (kwa mbele. Kila chumba kinatoshelew kuku 125 wa kutaga mayai au 250 wa nyama.
Vifaa Vinavyohitajika Katika Banda la Kuku
Vifaa vinavyohitajika ni kama vile vyombo vya maji, chakula, viota, vifaa vya kupumzikia, kulelea vifaranga na vyombo vya kuongezajoto.
· Vyombo vya Maji:
Kuna vyombo maalum vya plastiki au bati vya kuwekea maji kwa ajili ya vifaranga.
Vyombo hivi hupatikana katika maduka yanayouza pembejeo na vifaa vya kilimo.
Kama vifaa hivi havipatikani tumia sahani na makopo.
Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza maji katika kopo halafu litunike kwa sahani na ligeuze.
Pia kuna vyombo vya maji kwa ajili ya kuku wakubwa.
Vyombo hivyo ni kama vyombo maalum vya bati na plastiki, madebe, vyungu, sufuria, karai na vibuyu vilivyokatwa vizuri.

 
Chombo cha bati cha kuwekea maji

Vyombo Vya Chakula:
Vyombo vya chakula vya vifaranga ni chano za mayai, makasha yaliyobebea vifaranga na vyombo maalum vya bati au plastiki. Chano za mayai na makasha yatumike kwa juma la kwanza tu. Vyombo vya chakula kwa ajili ya kuku wakubwa ni vile vilivyotengenzwa kwa mbao au bati.

 
Chombo cha bati cha kuwekea chakula

 

 
Chombo cha mbao cha kuwekea chakula

Viota
Kuna aina mbili za viota ambavyo vinatumika kwa ajili ya kutagia mayai, aina ya kwanza ni kiota cha kuku mmoja mmoja. Kila kiota kinaweza kutumiwa na kuku watano kwa zamu. Vipimo vya kila kiota viwe na sentimita 30 upana, sentimita 30 urefu na sentimita 35 kina. Upande wa mbele uachwe wazi lakini sentimita kumi za kwanza kutoka chini zizibwe kwa mbao.

 
Kiota cha kuku mmoja

Aina ya pili ya kiota ni ya kiota chajumla. Kiota hiki kinaweza kutumiwa na kuku watano hadi sita kwa mara moja. Vipimo vya kiota hicho ni sentimita 30 upana, sentimita 150 ur.efu na sentimita 55 kina.

 
Kiota cha kuku wengi

Sifa za Kiota
– Kiwe na giza kiasi. Giza hupunguza tabia ya kuku kula mayai au kuonoana
– Kiwe kimewekwa mahali ambako ni rahisi kwa kuku kuingia ma kutoka, pia kusafisha.

 

Leave a Reply