Upungufu wa vitamini hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin. Sio kila ugonjwa unao uona katika kuku, kanga, na hata kware huenda kuwa umesababishwa na vimelea au virusi fulani.
UMUHIMU WA VITAMINI.
– Husaidia katika ukuaji wa kuku.
– Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka.
– Husaidia kuku kuwa mwenye afya.
– Huwezesha kuku kuwa mtagaji mzuri.
VITAMINI A
Huathiri zaidi kuku wadogo wanaokua, macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji, kuku wenye ukosefu wa vitamin A hawaponi na hatimaye hufa. Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi, Ukuaji wa manyoya huwa hafifu, ukuaji wa taratibu kwa kuku, Panga za kuku huonekana hafifu.
JINSI YA KUKABILIANA.
kinga ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara pia wape kuku wote dawa ya vitamin za kuku (Multivitamin) hili kuzuia kujitokeza kwa ugonjwa huu.
VITAMINI B
Manyoya huonekana kusambaratika, panga za kuku kuonekana zikiwa zimepauka, na kwa kuku watagaji hupunguza uwezo wao wa kutotoa mayai.
JINSI YA KUKABILIANA.
Wapatie kuku wako Dawa za multivitamin.
VITAMIN E
Hizi ni dalili za ukosefu wa vitamin E kwa kuku,
– shingo huanguka chini na kupinda.
– Vifaranga huanguka kifudi fudi.
– Utagaji wa kuku hushuka kwa kiasi kikubwa.
VITAMIN D
Ukosefu wa vitamin D hupelekea tatizo la mifupa kuwa laini, na hali hii hupelekea mifupa kupinda pia magoti huvimba na hata midomo kuwa laini. Na hata ukuaji wa kuku huwa wa hafifu.
Hii hutokana madini aina ya madini ya calcium na fosifolusi kutojengeka kwenye mifupa.
Kwa kuku watagaji hali hii hupeleka kwa kuku watagaji kutaga mayai yenye ganda laini.
JINSI YA KUKABILIANA.
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mimea, mfano majani ya lusina, mpapai, mchicha na mikunde
kazi ya vitamini ni kulinda mwili dhidi ya magonjwa, watu wengi hupenda kutumia vitamini mbadala za viwandani kuliko zile vitamini halisia ambayo imetokana na nguvu za jua na madini toka kwenye udongo ambayohupatikana kwenye majani, ni vyema ukaangalia vitu
MABORESHO YA VITAMINI KWA KUKU.
VITAMINI
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mimea, mfano majani ya lusina, mpapai, mchicha na mikunde