Imeeandikwa na watafiti B. A.Temba, F.K.Kajuna, G.S.Pango na R Benard kuchapishwa kwenye jarida (journal) la Livestock Research for Rural Development toleo la 28 (1) la Januari 2016 kwa lugha ya kiingereza

Kwa ufupi. Lengo la utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza matumizi ya taarifa na vyombo vya mawasiliano miongoni mwa wafugaji wa kuku na kubaini vitu vinavyozuia upatikanaji wake na utumiaji kwa wafugaji wa kuku. Taarifa za upatikanaji wa huduma za kigani kwa wafugaji ni muhimu sana ili kuongeza uzalishaji wa mifugo. Utafiti huu ulitumia madodoso kwa wafugaji wa kuku 160 kutoka kata nne za Manispaa ya Morogoro (Kata ya Mazimbu, Kilakala, Kihonda na Bigwa).

Utafiti huo ulibaini kuwa wafugaji wengi hutumia Luninga (TV), simu na redio kupata taarifa za kigani wakati wachache hupata taarifa toka kwenye mitandao, magazeti, vitabu, machaqpisho mbalimbali na vitu vingine vya kusikiliza au kutazama mfano CD na DVD zenye mafunzo ya ufugaji.

Utafiti umeonyesha kuwa wafugaji wengi (asilimia 82.5) hawapati taarifa wanazohitaji kulingana na ufugaji wanaoufanya. Vitu vinavyochangia wasipate taarifa wanazozihitaji ni pamoja na gharama kuwa kubwa, umeme usiokuwa wa uhakika, mawasiliano mabovu ya TV na radio na kukosekana kwa elimu juu ya matumizi ya vyombo vya kisasa vya kusambaza taarifa.

Hata hivyo matumizi vyombo vya mawasiliano ilionekana kwa kiasi kikubwa vina rahisisha upatikanaji wa taarifa za huduma za ugani kwa wafugaji. Matumizi ya taarifa hizo na vyombo vya mawasiliano vilionekana kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na kuongezeka kwa uzalishaji kwa wafugaji wa kuku. Kwa hiyo watafiti wamependekeza kuongeza mkazo zaidi ili kuwawezesha na kuwahamasisha wafugaji namna bora ya kutumia taarifa na vyombo vya mawasiliano kwenye ufugaji wao. Hii itawasaidia wafanye ufugaji unaoendana na wakati na kuongeza uzalishaji.

Chapisho zima: Kwa lugha ya kiingereza linapatikana hapa

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!