Upotevu wa kiuchumi unaotokana na kukataliwa kwa nyama au shehemu ya nyama na sababu za kukataliwa

Huu ni utafiti ulifanywa na C.Kiswaga, E.L. Mayenga (wa Halmashauri ya wilaya ya Same), F.V. Silayo (wa Halmashauri ya Korogwe mjini) na E.S.Swai (kutoka Wakala wa Maabara za Mifugo Tanzania, Temeke). Utafiti ulifanyika mwezi Novemba 2015 hadi Januari 2016 kwenye machinjio yaliyopo wilaya za Same (Kilimanjaro) na Korogwe (Tanga) na manispaa ya Temeke (Dar es Salaam). Lengo la utafiti huu ilikuwa ni kubaini sababu za kukataliwa kwa nyama au sehemu ya nyama ama viungo kama maini, figo, moyo n.k, ukubwa wa tatizo kwenye machinjio yetu na kukadria upotevu kiuchumi unasababishwa na kukataliwa huko kwa ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe.

Jumla ya ng’ombe 952, mbuzi 1133 na kondoo 811 toka Same, ngo’ombe 696, mbuzi 305 na kondoo 165 Korogwe na Nguruwe 516 toka Manispaa ya Temeke walichinjwa na kukaguliwa kwa umakini mkubwa kwa kutumia mwongozo wa ukaguzi wa nyama wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO).

Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kwamba sababu kubwa za kukataliwa huko kwa nyama toka kwa ng’ombe, mbuzi, kondoo ni kutokana na mifugo kuwa na magonjwa haya: Minyoo bapa (Fasciolosis), minyoo ya tegu (Cysticercosis), magonjwa ya ini (Hepatitis na Cirrhosis), Kichomi (Pneumonia), Majipu (Abscesses), kuvimba kwa bandama (Splenomegaly), ugonjwa wa moyo (Pericarditis) na magonjwa ya figo (Nephritis, Renal cysts, Hydronephrosis).

Ini - Upotevu wa kiuchumi unaotokana na kukataliwa kwa nyama au shehemu ya nyama na sababu za kukataliwa Cysts 300x225 - Upotevu wa kiuchumi unaotokana na kukataliwa kwa nyama au shehemu ya nyama na sababu za kukataliwa Cysts in heart 300x218 - Upotevu wa kiuchumi unaotokana na kukataliwa kwa nyama au shehemu ya nyama na sababu za kukataliwa

Jumla ya mapafu 103 (3.6%), utumbo 32 (1.1%), maini 81 (2.8%), figo 15(0.5%) mioyo 3 (0.1%) na bandama 30 (1.1) zilikataliwa kwenye machinjio wilayani Same. Wilayani Korogwe zilikataliwa jumla ya mapafu 244 (20.9%), maini 140 (12%), figo 127 (10.9%), miyo 61 (5.2%) na bandama 19 (1.6%). Kwa upande wa nguruwe manispaa ya Temeke figo 12 (2.3%), mapafu 10 (1.9%) na nyama yote ya nguruwe 10 (1.9%) ziliamriwa ziteketezwe wakati wa kuchinja. Aidha kati ya wanyama 843 majike waliochinjwa wilayani Same, 42 (4.9%) walikuwa na mimba, huku Korogwe ni wanyama 9 (3.8%) kati ya 240 na Temeke 9 (5.1%) kati ya 176 wanyama majike waliochinjwa walikuwa na mimba.

Upotevu huu wa nyama au viungo kukataliwa kwenye machinjio ulikadiriwa kuwa ni dola za Kimarekani 39,002.44 wilayani Same, dola 119,935.02 Korogwe na 46,791.56 manispaa ya Temeke. Lakini pia uwepo wa magonjwa yanayoenezwa na tegu (Cysticercosis) ni kiashiria hatari cha kuenea kwa ugonjwa huu kwa binadamu. Hii inafanya utafiti huu kuwa muhimu sana kwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma, kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kuweka njia stahiki za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu kwa binadamu. Hii inapswa kwenda sambamba na matumizi sawia ya sharia zinahusu ustawi wa wanyama na afya ya binadamu.

Chapisho zima kwa lugha ya Kiingereza lipo kwenye jarida la kila mwezi la Livestock Research for Rural Development toleo la 28 (11) la mwaka 2016 hapa 

Maelezo zaidi juu ya magonjwa yaliyotajwa hapo juu

  1. Minyoo bapa (Fasciolosis)- Namna ya kupambana nayo na kuzuia isiwapate mifugo yako soma hapa
  2. Minyoo ya tegu (Cysticercosis)- maelezo yake soma hapa

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!