HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO 2020/2021: MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI



 

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

NA MATUMIZI KWA MWAKA 2020/21




MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Hotuba hiyo iliyotolewa tarehe 11.06.2020 mbele ya bunge imeonyesha mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi kama ifuatavyo;


1. Sekta ya mifugo


1   Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mifugo ni pamoja na: 



   a)Kuongezeka kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho kufikia hekta milioni 2.82 Aprili 2020 kutoka hekta milioni 1.4 mwaka 2015. Ongezeko hili limewezesha kupungua kwa migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima nchini. 

   

   b) Sekta ya mifugo ilifanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 22 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo hakukuwa na mkopo kutoka TADB. 


     c) Ujenzi wa viwanda vya nyama vya Tan Choice Limited, Elia Foods Overseas Ltd, Binjiang Company Ltd na kiwanda cha kusindika maziwa cha Galaxy chenye uwezo wa kusindika lita 75,000 kwa siku umekamilika.


2. Sekta ya uvuvi


Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya uvuvi ni pamoja na: 


a)Kuongezeka kwa mauzo ya samaki nje ya nchi kufikia wastani wa shilingi bilioni 692 kwa mwaka kutoka wastani wa shilingi bilioni 379; 


b) Kuimarika kwa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini; 


c) Kuongezeka kwa samaki waliovuliwa kutoka tani 387,543 na kufikia tani 448,467; 


d) Kuongezeka kwa wingi wa samaki aina ya Sangara kutoka tani 417,936 mwaka 2015 hadi kufikia tani 816,964 mwaka 2020; 


d) Kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO); 


e) Kudhibiti uvuvi haramu kwa asilimia zaidi ya 80 katika maji baridi na asilimia 100 kwa uvuvi wa kutumia mabomu kwa ukanda wa pwani ya bahari;


f) Serikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji katika tasnia ya ufugaji samaki na kufanikiwa kuongeza idadi ya wafugaji samaki kutoka 18,843 hadi 26,474 mwaka 2020.


 

Leave a Reply