HABARINI NAKUMBUKA NATAKIWA KULETA SOMO LA MWANGA NITATEKELEZA LEO

Ila naomba twende sawa hapa wafugaji mkifaulu katika swala hili hamtakaa mjute wala kumlipa mfanyakazi wa kuhudumia kuku hela kidogo

MTUNZAJI WA KUKU BANDANI/stockmanship

Huyu ndiye mtu muhimu zaidi kwenye makuzi ya kuku kuliko hata wew mmiliki wa mradi kwani asipotekeleza majukumu yake ipasavyo hela yako itapotea bure

Unatakiwa kumfanya mtunzaji kuku awe kama sehemu ya mradi nae ajione hatumikishwi na aifurahie kazi

Mtunzaji wa kuku hapaswi kukalipiwa kila anapokosea anatakiwa kuelekezwa kwa upole ili ajue nini amekosea na afanye nini kwaajili ya kuboresha

Mtunzaji wa kuku ndie haswa anaetekeleza maagizo yote ambayo tumekua tulifundishana kuazia usafi..dawa..ulishaji..joto na mambo kadha wa kadha yanayohusu kuku kuliko wew mmiliki unaeshinda kazini

Mtunzaji wa kuku ndie mtu sahihi zaidi kuhudhuria semina na mafunzo mbalimbali ya kuku…kwani atafahamu umuhimu wa kilakitu kwanini kinafanyika na akitekeleza utaona matokeo hivyo ni vema kama utahudhuria mafunzo au semina yeye awepo au aje yeye wew ubaki

Mtunzaji wa kuku akikaripiwa au kufokewa kila Mara anahisi kutengwa na kunyanyaswa na atatekeleza majukumu ukiwepo ilaa ukiondoka atataka kulipiza kwa kuku na utapata hasara usiyojua inatoka wapi

Kubadilisha mtunzaji wa kuku kilaa wakati si suluhisho cha msingi apewe elimu aelewe mambo na umuhimu wake kwa undani

Mfano unaweza ukawa unacheza nae kosaikolojia tu kwamba kama utajitahidi kuongeza tray za mayai kila wiki atapata bonus ya tray za mayai kama kumpa hamasa ya kufanya kazi kwa moyo

Kumbuka hata kama wew ukipewa kazi ya kutunza kuku na huna taaluma kuku wamaweza kufa…kwahiyo usidhani kilaa kuku kufa bandani ni uzembe wa mfanyakazi kupelekea kumfukuza au kumkaripia mpaka akose hamu ya kukaa na kuku wako

Unaweza kuwa unamnunulia nguo au kumtoa OUT sikumoja moja akala vizuri kama unavofanya kwa watoto wako atajiona ni mmoja wa wanafamilia na sio kujiona mtunza kuku

Amini kama utayatekeleza haya machache kuku wako wataenda vema na uzalishaji utaongezeka maradufu

KWA MWELEWA ATAKUA AMEPATA SOMO KUBWA AMBALO NDANI YA MWEZI MMOJA ATAKUA ANAFURAHIA HILI SOMO

Imeandaliwa na
 Greyson kahise
 Mtaalamu wa kuku
 0769799728  0715894582

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!