MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA

ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga.

SIFA ZA KIFARANGA BORA
==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu.
==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka
==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga
==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema
==Kifanga awe na afya nzuri

VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA

==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea

==Angalia ubora wao..kama afya…kitovu…na ambao hawana shida.

==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality.

==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia thermometer,,,Weka rekodi ya vifaranga wenye afya kamili walio bakia.

==Kwa wiki la kwanza siku 7 joto kubwa la banda liwe kuanzia nyuzi joto 30- 35 na joto la chini lisipungue 28°C.

==Hakikisha vyombo vyote vipo,,,,Maranda yapo..na mwanga upo…pia mifuko itandikwe chini kuwawezesha vifaranga
 kuona chakula.

VITU VYA KUZINGATIA BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA

==Joto la bandani liwe kama ilivyo elekezwa hapo juu.

==Chakula na maji viwepo kwa masaa 24 kwa siku 14-21 za mwanzo,,,,kisha ondoa chanzo cha joto na taa zizimwe usiku.

==Wiki la kwanza kati ya siku ya 7 au ya kumi vifaranga wapewe chanjo ya kideli/newcastle

===Siku ya 14 au ya 18 kuku wapewe chanjo ya GUMBORO/IBD

==Muda huu wa wiki tatu wape chakula aina na Starter crumble…au siku saba za mwanzo wape Pre-starter alafu wiki 2 wape starter.

==Hudhuria mara kwa Mara bandani kuangalia tabia za vifaranga wako…ambapo ,,,

Joto likizidi vifaranga watasogea mbali na chanzo cha joto/pembezoni.

Joto likipungua vifaranga watasogea kwenye chanzo cha joto au kurundikana sehemu moja….hiii inaweza kupelekea vifaranga kufa….

Upepo ukizidi vifaranga watakimbia eneo upepo unapotokea na watakua wakizunguka zunguka kwa makundi bandani

Joto likiwa sahihi vifaranga watatawanyika banda zima na wataendelea kula na kunywa maji.

KUMBUKA UKIKOSEA JOTO VIFARANGA WENGI WATAKUFA NDANI YA MUDA MCHACHE

==Hakikisha vifaranga wako wanakula na kunywa maji safi sawa na Yale unayoyatumia wewe….wakionesha udhaifu unaweza waongeza Glucose..sio lazima….pia unaweza kuwawekea Multivitamins kwa kutegemea chakula ulicho wapa.

==Hakikisha mzunguko wa hewa ni mzuri kuzuia gesi chafu ya carbon monoxide ambayo husababisha vifaranga kulala chini na kushindwa kunyanyuka.

==Hakikisha maranda ni makavu muda wote kwa kuyageuza geuza Mara kwa Mara kuzuia ugonjwa wa COCCIDIOSIS

IMEANDALIWA NA MR GREYSON KAHISE MTAALAMU WA KUKU 0769799728.

Leave a Reply