Serikali imefunga mtambo wa kuchakata mazao ya nyuki kwa kiwango cha kimataifa wilayani Manyoni mkoani Singida. Kiwanda hiki kilichomalizika kufungwa kitakuwa na uwezo wa kuchakata asali lita 500 kwa siku.
Kiwanda hiki kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye misitu ya eneo la Itigi lakini pia wananchi wanaruhusiwa kukitumia kuchakata mazao yao binafsi.
Ufungaji wa mtambo huu ambao kwa jumla umegharimu takribani milioni 80 unategememewa kuondoa tatizo la ubora duni wa asali na nta katika ukanda huu na maeneo ya jirani yatakayo nufaika na uwepo wa mtambo huu.
Kwa sasa uwekezaji mkubwa unaendelea katika misitu ya Aghondi na Kilinga ili kuongeza uzalishaji wa asali.
Tumia asali, fuga nyuki na hifadhi misitu. Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TFS (Tanzania Forest Service Agency) Prof. Dos Santos Silayo.
Soma zaidi kuhusu ufugaji wa nyuki kupitia viunganishi hapa chini
1. UFUGAJI WA NYUKI KWA NJIA YA KISASA