Kudonoana na kula mayai

MAKALA KUHUSU KUKU KULA MAYAI, KUDONOANA NA KUNYONYOKA MANYOYA

Tatizo la kuku kuwa na tabia zisizo faa/cannibalism limekua shida kubwa kwa wafugaji wengi wa kuku aina zote, ilaa limekua likijitokeza sana hasa kwa kuku wa mayai

Tatizo hili pia limekua likijitokeza kwa kuku wa rika tofauti tofauti..ilaa linazidi pale kuku wanapo anza kutaga mayai

Chanzo cha tatizo

Kuku kuwa wengi kwenye banda dogo kuzidi uwezo wa banda kuhifadhi kuku

Kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya chakula na maji pia kuku kukosa chakula cha kutosha

Upungufu wa protini, na madini kama calcium kwenye chakula cha kuku

Kuwa na idadi kubwa ya majogoo bandani kuzidi idadi inayotakiwa

Kuku kuchoka au kuzeeka pale muda wake utakapo kua umefika mwishoni

SULUHISHO

Kwa kuku anaekula mayai, mwongezee kiwango cha chakula chenye protein kwenye chakula kama soya meal na dagaa,,,pia mwongezee vitamins kuku wako atapunguza kula mayai pia waongezee kiwango cha mifupa au chokaa kwenye chakula chao,,kama utatumia magamba ya konokono hakikisha usalama wake maana wakati mwingine hupelekea Typhoid

Kwa kuku wanao donoana, weka kiwango sahihi cha vifaa vya maji na chakula, weka idadi sahihi ya kuku bandani wapate nafasi, wawekee majani muda fulani ili chakula kikiisha wawe busy kula wasipate muda wa kudonoana

Kwa kudonoana na kula mayai..endapo utatumia mbinu zote hapo juu na isisaidie njia ya mwisho kabisa ni kuwakata kuku midomo kwa kutumia kifaa maalumu cha kukatia midomo de-beacker…au kuchoma mdomo kwa njia za kienyeji…baada ya kuwakata midomo wape chakula kingi na vitamins kwa wingi

Kwa kuku wanao nyonyoka manyoya, waweke jogoo kwa uwiano na tetea,,jogooo mmoja kwa tetea 8-10, wape chakula chenye mchanganyiko wa madini ya calcium, zuia wadudu kama utitiri viroboto au kupe kwa kupulizia dawa ya Akheri powder au Paranex piaa usafi bandani uwe wakuridhisha.

Kikubwa cha kufahamu hapa ukifuatilia kwa makini hizi changamoto huwapata zaidi kuku ambao wafugaji hujichanganyia chakula chao, hivo ni vema ukachanganya chakula kutokana na uhitaji wa kuku na umri wa kuku na utumie formula sahihi ya mchanganyiko wa chakula

Imeandaliwa na Greyson Kahise mtaalamu wa kuku 0769799728…Karibu nikuhudumie kwa uzalishaji bora wa kuku na mayai

 

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!