Kwanini uongeze Lysine au Methionine ya Viwandani kwenye chakula cha kuku?

Pakua app ya Tovuti hii ya Ufugaji HAPA

Na Augustino Chengula

Neno protein siyo geni machoni pa wafugaji karibu wote maana limekuwa likitumika hata kwenye vyakula vya binadamu. Kuku wa aina zote kuanzia wa kienyeji, wa kisasa, wa mayai na nyama wanahitaji chakula chenye mchanganyiko wa protein. Kulingana na umuhimu wake chakula chochote kinapotengenezwa kwa ajili ya kuku lazima kizingatie uwiano wa protein. Mimea hasa mbegu za mahindi na soyabeans zina mchanganyiko wa proteins mbali na vitu vingine kama sukari, wanga na nyuzi nyuzi.

Protein imeundwa na mnyororo wa vitu vya thamani vinavyojulikana kama amino acics. Zipo amino acids za muhimu 20 kwa ajili ya utengenezaji wa protein kwenye mwili wa mnyama na bila hizo mnyama yeyote hawezi kuishi maana mwili wake utabomolewa. Mpangilio wa hizi amino acids 20 hujiunga kwa namna tofauti tofauti kutengeneza protein za aina tofauti tofauti mwilini. Kwa ufupi ni kama matofauti ya aina tofauti tofauti yanavyopangwa wakati wa kujenga nyumba.

Matumizi ya amino acids ya viwandani kwa ajili ya kuwaongezea kuku yalianza mwishoni mwa miaka ya 1950 na 1960 ambapo Lysine na Methionine zilianza kutengenezwa kwa ajili ya kuchanganya kwenye chakula cha kuku. Baadaye mwishoni mwa miaka ya 1980 Threonine na Tryptophan nazo zilianza kutengenezwa ili kuongeza ubora wa utumiaji wa protein mwilini mwa kuku na kuleta matokeo chanya mapema. Soyabeans zimekuwa zikitumika sana kwenye mchanganyiko wa chakula cha kuku kwani ina protein nyingi ukilinganisha na vyanzo vingine kama nafaka zenye asilimia takribani 10 hivi. Lysine na Methionine ndizo amino acids mbili ambazo zimekuwa zikiongezwa kwenye chakula cha kuku.

Swali linalowajia wafugaji wengi wa kuku, kwanini waongeze virutubisho hivyo (Lysine au Methionine) vya ziada kwenye chakula cha kuku ambavyo ni gharama badala ya kuongeza soyabeans ambazo zina amino acids hizo? Jibu rahisi ni kwamba virutubisho hivyo (20 amino acids) kwenye vyanzo mbalimbali kama soyabeans na vingine havipo katika uwiano sawa. Hii inatokana na kwamba protein kwenye mazao hayo ipo katika mchanyiko tofauti tofauti na hivyo kufanya hata hivyo virutubisho kuwa tofauti tofauti. Hivyo wakati kuku wanabadili protein kutoka kwenye soyabeans kwenda kwenye nyama na mayai kunakuwa hakuna uwiano sawa kwa amino acids zote 20 za muhimu kwa kuku. Na tafiti ambzao zimekwisha fanyika zinaonyesha kuwa kuku pamoja na Wanyama wengine wanahitaji zaidi lysine na methionine kuliko ile iliyopo kwenye mahindi na soyabean inayotumika kutengeneza mchanganyiko wa chakula tunachowalisha kuku. Kumbuka proteini inatumika kujenga mwili wa kuku (nyama) na mayai na proteini inatengezezwa na amino acid zote 20 kwa mchanganyiko wa aina yake. Hivyo kwa lugha rahisi ufpungufu wa virutubisho hvi viwili vya muhimu kutazorotesha ukuaji wa kuku na utagaji wa mayai. Hivyo unavyodhani kuwa kununua Lysine na Methionine ni gharama kwa ajili ya kuongeza kwenye chakula cha kuku, kiuchumi ni faida zaidi ukinunua kuliko ukiacha.

Haina sababu kuongeza amino acids zote 20 wakati zilizopungufu kwenye vyanzo vya vyakula vya kuku ni hizo mbili tu wakati kwa kuongeza hizo mbili tu tunakuwa na uhakika mahitaji ya virutubisho vyote yatatimia na kiuchumi itakuwa na tija zaidi. Lysine ndiyo amino acid ambayo imeonekana kuwa pungufu kwenye vyakula vingi wanavyopewa mifugo hasa kuku na nguruwe ndo maana inashauriwa kuongezea ya ziada.  Lysine ikichanganywa kwenye chakula cha kuku mara kwa mara, kuku watakuwa haraka, wakiwa na afya nzuri na wa kutaga mayai wataongeza utagaji.

 

Leave a Reply