- Utangulizi
Ufugaji wa samaki ni ukuzaji wa samaki katika mabwawa, matenki n.k
Mseto wa ufugaji wa samaki, kuku na kilimo cha mzao ya kilimo (Integrated Aquaculture agriculture -IAA) ni kilimo kinachohusisha zaidi ya zao moja (yaani samaki, kuku na kilimo cha mazao) kaitka eneo moja kwa lengo la kumrahisishia mfugaji kufuatilia na kutumia muda vizuri, kutumia eneo dogo la ardhi kuongeza kipato na kuku uchumi wa kaya.
Katika ufugaji huu samadi ya kuku hudondoka katika bwawa la samaki na kuchochea kuota kwa mwani (Uoto wa asili wa kijani) ndani ya bwawa ambacho ndicho chakula cha samaki, lakini pia maji yanayotumika bwawani yanakuwa na virutubisho vingi. Maji haya hutumika kumwagilia mazao ya kilimo na kuchochea ukuaji mzuri wa mazao ya kilimo/mbogamboga.
Lengo kuu la kuanzisha tekinolojia ya kilimo mesto ni kuwezesha shughuli zote kufanyika katika eneo moja kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazo (samaki, kuku na mbogamboga) katika eneo dogo la ardhi kuziwezesha jamii za wa wafugaji kupata kipato, lishe bora na mazao zaidi ya moja katika eneo moja.
- Umuhimu wa Ufugaji/kilimo mseto
- Kumfanya mkulima kupata mazao zaidi ya moja katika eneo moja dogo kwa wakati tofauti (yaani mayai, kuku, samaki na mazao ya kilimo)
- Kupunguza hasara hasa wakati wa zao moja halifanyi vizuri, mkulima anaweza kupata mavuno yanayotokana na mazao mengine
- Lakini pia husaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na kumwaga maji machafu, yanayotoka ndani ya bwawa wakati wa kubadilisha, badala yake maji yanatumika kumwagilia mazao ya kilimo/mbogamboga
- Hupunguza matumizi makubwa ya rasilimali na gharama ya uzalishaji mzao.
Badala ya kukununua chakula kingi kwa ajili ya kuku na samaki, mfugaji atanunua chakula kidogo kwa ajili ya kuku na samaki wataongezwa chakula kidogo na pia mbolea kutoka kwenye bwawa la samaki inatumika kurutubisha mazao ya kilimo.
- Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kuibiwamazao shambani, kwa sababu muda mwingi mkulima anakuwa eneo moja akihudumia shamba lake la mseto.
- Pia kilimo mseto huongeza mavuno zaidi, kutokana na utafiti uliofanyika na Wataalamu wa chou kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu ch Sokoine cha Kilimo (SUA) unathibitisha kuwa mbolea inayotokana na kuku inakuwa na virutubisho vingi na kusababisha uoto wa asili ndani ya bwawa kuota kwa wingi ambacho ndicho chakula cha samaki, samaki wanakua haraka na uzito mkubwa, lakini pia maji yanayotoka kwenye bwawa yanakuwa na virutubisho vingi na huchochea kustawi vizuri kwa mazao ya kilimo.
- Nini cha kuzingatia wakati unafikiria kuwekeza katika kilimo mseto
- Kuweka mipango mizuri na udhibiti bora
- Uchaguzi wa eneo zuri la kuchimba bwawa lenye udongo mzuri wa mfinyanzi, maji safi nay a uhakika, eneo linalofikika kwa urahisi na eneo lenye mwinuko wa wastani.
- Kutumia mbegu bora na chakula cha mifugo na pia kuzingatia mchanganyiko wa chakula kwa ajili ya kuku na samaki. Uwepo wa wafanyakazi/vibarua katika eneo husika.
- Usimamizi mzuri wa bwawa ili kuhakikisha vimelea vya magonjwa pamoja na viumbe waharibifu kama nyoka na kenge wasifike kwenye bwawa kwa kuweka uzio.
- Mahali pa kupata mbegu bora ya samaki aina ya Perege na Kambale kwa ajili ya kufuga
- Ili kupata mbegu bora za samaki unaweza kuwasiliana na Idara ya ukuzaji viumbe kwenye maji iliyo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Halmashauri za Wilaya na Vituo vya Serikali vya uzalishaji wa samaki vilivyopo maeneo mbalimbali nchini mfano Kingolwira mkoani Morogoro.
IMEANDALIWA NA
IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUFIJI
- L. P 28
UTETE/RUFIJI