Na Godwin Magambo
Leo nawaletea makala kuhusu utengenezaji wa chakula cha kuku wa mayai (Layers, Kuroilers)
Utengenezaji wa chakula cha kuku kwa kutumia fomyula sahihi ni njia nzuri kwa mfugaji ya kupunguza gharama za mradi wake wa kuku, pia kuhakikisha chakula kinakua na virutubisho muhimu kwa usahihi.
Ifuatayo ni fomyula ya utengenezaji wa chakula cha Kuku: Starter, Grower na Finisher.
——————————
- CHICKS STARTER, WIKI 1 – 5
- Pumba za maindi 41kg
- Dagaa walio sagwa 5kg
- Mtama ulio sagwa 25kg
- Mashudu ya alizeti 22kg
- Chumvi 0.5kg
- Damu iliyo sagwa 3kg
- Unga wa mifupa 2kg
- Methionine 0.25kg
- Prexix 0.5kg
- Vitamins 0.5kg
- Lysine 0.25kg
TOTAL =100KG
——————————
GROWER MASH, WIKI 6 – 16
- Mashudu ya alizeti 22kg
- Ngano nzima 5kg
- Dagaa walio sagwa 11kg
- DCP 1kg
- Unga wa mifupa 5kg
- Chokaa 2kg
- Chumvi 0.5kg
- Mahindi yaliyo parazwa 10kg
- Premix 0.5kg
TOTAL =100KG
——————————
LAYERS MASH WIKI 17
- Mashudu ya alizeti 20kg
- Pumba za mahindi 35kg
- Chokaa 3kg
- Mtama 6kg
- Dagaa walio sagwa 12kg
- Unga wa mifupa 5kg
- Damu iliyo sagwa 5kg
——————————
Njia rahisi ya kujitengenezea chakula chako nyumbani kwa viambata vinavyopatikana mtaani kwako.
Tengeneza kilo 100 kwa kanuni hizi
Chick mash
chakula cha kuku kuanzia siku 1 hadi wiki 8 changanya:
Pumba laini za mahindi kilo 40
Mashudu ya alizeti kilo20
Pumba za mtama kilo 27
Chokaa ya mifugo/unga wa mifupa kilo 2 na robo
Dagaa kilo 10
Chumvi nusu kilo
Premix /broiler premix robo kilo
Growers mash miezi 2 – 4
Mahindi yaliyobarazwa kilo 25
Pumba za mahindi kilo 44
Mashudu ya alizeti kilo 17
Chikaa ya mifugo kilo 3 na robo
Dagaa kilo 10
Chumvi robo kilo
Broler premix nusu kilo
Growers finisher miezi minne hadi mitano
Mahindi yaliyo barazwa kilo 31
Mashudu ya alizeti kilo 18
Pumba za mahindi kilo 38
Chokaa kilo 2 na robo
Dagaa kilo 13
Brioler premix robo kilo
Chumvi nusu kilo.
Kuku wanaotaga miezi 6+
Dagaa kilo 12
Mahindi yaliyo barazwa kilo 30
Mtama kilo 6 na robo tatu
Mashudu ya alizeti kilo 20
Pumba za mahindi kilo 23
Chumvi robo kilo
Chokaa ya mifugo kilo 3
Unga wa mifupa kilo 5
Layers premix robo kilo
MUHIMU
– Hakikisha unachanganya vizuri ili kupata mchanganyiko wenye uwiano Sahihi wa virutubisho.
– Chakula kihifadhiwe vizuri ili kuzuia unyevu.
– Kuku wapewe chakula kwa kiasi kulingana na umri na idadi yao.